MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA HUU YATANGAZWA

Jumla ya wanafunzi 567,567 wamefaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011na watafanyiwa mtihani wa majaribio kabla ya kuanza masomo yao rasmi katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza matokeo hayo (leo), jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (Mb.) amesema, utaratibu huo wa kufanyiwa majaribio utaanza mwakani 2012, ambapo wanafunzi waliofaulu watafanyiwa majaribio ya kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Wakati huo huo, Baraza la Mtihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa 9,736 sawa na asilimia 1.0 waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo.

“Mwanafunzi atakayebainika kuwa kajiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Mulugo.

Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu alisema kimeongezeka hadi kufikia asilimia 58.28 ukilinganisha na cha mwaka jana ambacho kilikuwa asimilia 53.52.

Aliongeza kuwa kiwango cha ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hesabu kimepanda . Somo la Kiingereza kutoka asilimia 36.47 mwaka jana hadi asilimia 46.70 kwa mwaka huu , wakati somo la Sayansi ni asilimia 61.33 mwaka huu toka asilimia 56.05mwaka jana na Hesabu asilimia 39.36 mwaka huu toka asilimia 24.70mwaka jana.

Jumla ya wanafunzi 983, 545 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi wa Septemba 2011 na kuonesha kuwa, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 mwaka jana hadi 58.28. Jumla ya wasichana waliofaulu ni 27,377 na wavulana ni 289,190.

Wakati huo huo, Serikali imesema, kazi ya kuhakiki madai ya walimu imekamilika tangu Desemba 2, mwaka huu na kwamba madai hayo ni kiasi cha sh. bilioni 52.

Akijibu swali lililoulizwa na waandishi kuhusu madai ya walimu, Naibu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 ni za mishahara na bilioni 22 ni za madai mengineyo.

Bw. Gesimba ameongeza kuwa, madai ya malipo mengine yataanza kulipwa mwezi huu (Desemba) na madai ya malipo ya mishahara yatalipwa ifikapo Januari 2012.

Hata hivyo alisema tayari Hazina wameshalipa bilioni 28 za madai ya mishahara kuanzia Julai mwaka jana hadi Novemba mwaka huu.

Na Gradys Sigera & Magreth Kinabo – MAELEZO

About these ads

26 responses to this post.

 1. Vp kwa wale ambayo hawajui kusoma na kuandika!?

  Reply

 2. Posted by JOHARI SALUM on December 3, 2012 at 11:05 pm

  MORINGE

  Reply

 3. Mbona hayo matokeo siyaonii!

  Reply

 4. Posted by geofrey anthony mbegu on December 13, 2012 at 3:28 pm

  matokeo ya shule za msingi mwaka 2012-2013 yanatoka lini

  Reply

 5. Posted by ceci on December 13, 2012 at 5:08 pm

  matokeo mmetanganza mbona hatuyaoni …

  Reply

 6. Posted by issajuma on December 14, 2012 at 10:58 am

  matokeo mbona hayaonekani

  Reply

 7. Posted by Ezekiel Masebo on December 19, 2012 at 5:54 am

  Uo ni uzushi mbona hayaonekani?

  Reply

 8. naomba kutumiwa matokeo ya darasa la nne 2012

  Reply

 9. hata mimi siyaoni

  Reply

 10. Posted by JULLIUS MAFURU on December 20, 2012 at 6:33 pm

  Hayo matokeo ya darasa la saba 2012 yametangazwa ya SHUKRU KAWAMBA TBC, mbona hamja yapost kwenye mtandao????? kulikoni????

  Reply

 11. Posted by doreen on December 21, 2012 at 5:04 am

  mbona matokeo yenyewe hamjaweka, mnatakiwa kujipanga ukitangaza kitu means watu wanataka waone

  Reply

 12. Posted by Eunice on December 21, 2012 at 6:40 am

  matokeo mbona hayaonekani?

  Reply

 13. Posted by ernest ngomale on December 21, 2012 at 10:37 am

  jaman mungu awasaidie hawa watoto wafaulu wote na pia shule ya msingi iwambi mbeya daaa nawaombea sana

  Reply

 14. Posted by pankrac mbawala on December 21, 2012 at 2:51 pm

  NAOMBENI MATOKEO YA PANKRAC MBAWALA BUNJU A DAR ES SALAAM

  Reply

 15. Posted by VICENT on December 21, 2012 at 3:23 pm

  HAYO MATOKEO MBONA HAYAPO NET AU?

  Reply

 16. Posted by sabas rutole on December 21, 2012 at 5:20 pm

  Kwanini matokeo hayo hayaoneshi majina ya wanafunzi !Awamu ya pili sasa inakuwaje/Kulikoni?!

  Reply

 17. Posted by ally abdallah on December 21, 2012 at 9:18 pm

  kudadadekhi matokeo gani haya mpaka batani zangu zimebanduka.

  Reply

 18. naomba matokeo ya gadiel andrew mrinji na epiphany wilbard kaishe

  Reply

 19. Posted by manase barabona on December 22, 2012 at 11:20 am

  matokeo ya kwapi mbona 2natazamana 2 buree ha2yaoni

  Reply

 20. Posted by yahaya ismael on December 22, 2012 at 12:41 pm

  Mbona hayaonyeshi majina..shule walizosoma nk…Tz uchakachuaji ni kila mahali.

  Reply

 21. Posted by zulfa kakombe on December 22, 2012 at 5:12 pm

  matokeo jamani

  Reply

 22. Posted by yahaya on December 22, 2012 at 6:40 pm

  Mbona majibu ya darasa la saba munayachelewesha tunahitaji kujiandaa mapema huu wakati ni mgumu

  Reply

 23. Naomba matokeo ya shule ya msingi mwemage [ k]

  Reply

 24. Posted by jackobu on December 24, 2012 at 5:25 pm

  jamaani mbona matokeo hatuyaoni au si yawatanzania leo ni siku ya tatu katika mtandao tuna ona vichwa tu MATOKEO YATOKA au kiini macho

  Reply

 25. wachani uzushi. Tafadhalini mjipange ili mkitangaza matokeo na kwenye mtandao nako yawepo. Tanzania ya sasa si kama ya mwaka 47.

  Reply

 26. Tatizo nini baraza la mitihani wekeni hazalani matokeo

  Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 8,300 other followers

%d bloggers like this: