Archive for May, 2013

BREAKING NEWS: LWAKATARE AFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI, ABAKIZA SHITAKA MOJA


 

 

Wilfred Lwakatare (wa pili kulia) akipelekwa rumande. (Picha na maktaba yetu)

-Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
-Lwakatare amebakiza kesi moja tu ambayo ni kujaribu kumwekea sumu mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaki ambayo ina dhamana.
-Mmoja wa mawakili wa Lwakatare, Peter Kibatara, amesema kuwa kesi hiyo iliyobaki ni nyepesi, aahidi kumwekea dhamana Jumatatu ijayo.
-Wafuasi wa Chadema wachekelea.Chanzo:www.globalpublishers.info

SKENDO MTEGO WA KUJIUZA… AUNTY LULU ABADILIKA


Na Gladness Mallya
AMINI usiamini Global Publishers ni mtambo wa kurekebisha tabia! Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.

Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Katika ‘exclusive interview’ na paparazi wetu jijini Dar, juzikati, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
Alisema kuwa anawashukuru waandishi wa habari wa magazeti ya Global Publishers kwani wamebadilisha maisha yake, kama siyo wao angefikia hatua mbaya lakini kwa sasa ametulia na anafanya mambo ya maendeleo tofauti na zamani ambapo alikuwa hajielewi anafanya nini.
“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.
Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.
Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake  ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.Chanzo:www.globalpublishers.info

BREAKING NEWS: RUFAA DHIDI YA ZOMBE YATUPILIWA MBALI


Abdallah Zombe.

MAHAKAMA ya Rufaa nchini leo imefuta rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi, Abdallah Zombe, baada ya mahakama kujiridhisha kuwa hati ya kukatia rufaa hiyo ilikuwa na mapungufu.Chanzo:www.globalpublishers.info

MTANZANIA:SODA NI SUMU , HUSABABISHA KANSA, KISUKARI, MAGONJWA YA FIGO,SHINIKIZO LA DAMUHUATHIRI INI, INAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME


7 70fa9

HANA MIGUU, HANA MIKONO, LAKINI ANAFANYA MAMBO KUKUZIDI WEWE..!


 GOD IS GREAT

WABUNGE WAANZA KUJIHAMI NA MILIPUKO YA MABOMU….WAMEOMBA ULINZI UIMARISHWE BUNGENI


 

 

MBUNGE  wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.

 
Ndasa aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu kurushwa katika sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.
 
“Mheshimiwa Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana hofu ya kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa hafifu,” alisema Ndasa.

Ndasa alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha hivyo ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara makubwa kwa taifa.
 
Wabunge leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KWA BOMU KANISANI OLASITI WANAOTIBIWA HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA


 

mo2 90681

Taswira wakatia Rais Kikwete alipotembelea hospitali ya Mount Meru Mei 7, 2013 kufariji majeruhi wa mlipuko wa bomu katika kanisa la Olasiti jijini humo Jumapili iliyopita

 

mo4 1dcf1

mo6 a32bf

mo7 72d03

 

Bomu Arusha: Pengo afichua siri


 

 

 

Dar es Salaam/Arusha. Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
 
Kadinali Pengo
 
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
 
“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.
 
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
 
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.
 

 

TCU WAKIFUNGIA CHUO CHA KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY ( KIU ) KWA KUTOKIDHI VIGEZO


Image

 
CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo; 1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam. 2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu…

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa Amkabidhi kadi ya Uanachama aliyekuwa msaidizi wa Mbunge wa Iramba Magharibi-CCM, Mwigulu Nchemba Edgar Ntunda


 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, akimkabidhi kadi ya Uanachama aliyekuwa msaidizi wa Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM) Edgar Ntunda, baada ya kujiunga na Chadema jana. Picha na Fidelis Felix
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 4,662 other followers

%d bloggers like this: