Sitta: Taifa Lina Viongozi Wenye Sura Mbili


Sitta: Taifa Lina Viongozi Wenye Sura Mbili

Tumaini Msowoya, Iringa
WAZIRI wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema taifa linakabiliwa na viongozi wenye sura mbili ambao ni wale wasio waadilifu wanaofikiri kwa kutumia matumbo kwa kujilimbikizia mali na viongozi wachache wanaofikiri kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Sitta alisema hayo alipokuwa akitoa mada katika katika maadhimisho ya Siku ya Sheria kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, alipozungumza na Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, mjini Iringa (IUCo) jana.

Mada hiyo ilihusu mbinu za kisheria na utoaji wa huduma za kisheria Tanzania, ambapo Sitta alisema matatizo ambayo yanayolikabili taifa yanatokana na sura za viongozi wanaoliongoza.

Akifafanua, alisema wapo baadhi ya viongozi wabinafsi na wasio waadilifu ambao mara zote wamekuwa wakifikiri namna ya kujilimbikizia mali badala ya kuwatumikia watanzania.

“Msishangae, tuna viongozi wenye sura mbili, wapo wanaofikiri kwa kutumia matumbo yao jinsi ambavyo wataneemeka na kujinufaisha wenyewe, hawa ni wale wabinafsi lakini wapo viongozi ambao wanatumia ubongo katika kufikiri jinsi ambavyo watatumia uwezo wao wote katika kuwatumikia wananchi, mimi ni miongoni mwa hawa,” alisema Sitta.

Alisema taifa lina kazi kubwa ya kufikiri jinsi ya kumpata Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kwa madai kuwa ana kazi kubwa ya kuliondoa taifa mahali ambako limefikia kwa sasa sambamba na kuvunja makundi yote yaliyopo.

Alidai kuwa imefika wakati ambao lazima viongozi waweke bayana mali wanazomiliki ili wananchi wazitambue na kuwapima viongozi hao kulingana na kipato chao.

Aliongeza kuwa viongozi wengi wamesahau falsafa ya ‘Utu na Usawa’ iliyoanzishwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa tabaka kubwa miongoni mwa jamii.

Alisema wakati akiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, anajivunia jinsi ambavyo Bunge hilo liligeuka la wananchi na kuwajibika pale lilipotakiwa kufanya hivyo.

Kuhusu azimio la Arusha, Sitta alisema kuwa lilikuwa na umuhimu wake kwani lilionyesha namna kiongozi anapaswa kuwajibika, kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Akizungumzia Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sitta aliwataka watanzania kuondoa hofu juu ya kuwepo kwa soko la pamoja la jumuiya hiyo kwa madai kuwa tayari yameandaliwa mazingira mazuri ambayo yatawawezesha wananchi kuwepo katika soko hilo bila wasiwasi.

Alisema wapo katika majadiliano juu ya kuanzishwa kwa shirikisho la kisiasa ambapo tayari baadhi ya wanasheria wameajiriwa kwa ajili ya kushughulikia jambo hilo.

Aidha aliwataka vijana kujiamini na kutoogopa kuomba kazi katika nchi yoyote ndani ya jumuiya hiyo, badala ya kuendelea kunung’unika juu ya kukosekana kwa ajira.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Profesa Seth Nyagawa alisema njia pekee ya kuwakomboa watanzania katika umaskini ni kuwanoa ili waweze kuingia kiuhakika katika soko la pamoja la Afrika Mashariki, ikiwemo kuwaandaa kielimu.

Awali, mmoja wa wakufunzi wa Sheria chuoni hapo, Edward Nduguru alisema matatizo mengi yanayowakabili watanzania kwa sasa yanaweza kumalizwa na watanzania wenyewe pale watakaposhirikishwa katika maamuzi huku akiishauri Tume ya Katiba mpya kuhakikisha inakusanya maoni kwa makundi yote.
Chanzo: Mwananchi

HABARI MBALIMBALI KTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MGUU TFF


HABARI MBALIMBALI KTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MGUU TFF

ASPIRE KUANZA KUSAKA VIPAJI MEI 21
Mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu.
Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata.

Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.

TWIGA STARS KUJIPIMA KWA BANYANA BANYANA
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) itakayofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

UJAUZITO WA LULU…


UJAUZITO WA LULU...

Stori: Shakoor Jongo

BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kusekwa ameufungia kazi ujauzito wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuibuka na kueleza mkakati utakaomuwezesha kuikomboa damu ya mwanaye.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juzi, mzee huyo alisema yeye kama baba wa marehemu Kanumba, endapo maelezo ya kwamba Lulu ana ujauzito wa mwanaye yatafikishwa kwake, hawezi ‘kuchomoa’ ila atatumia dawa za kimila ‘DNA ya Kisukuma’ kubaini ukweli.

“Unajua hili suala la ujauzito wa Lulu linazidi kukua kila kukicha sasa mimi nitamaliza ubishi endapo nitakabidhiwa huyo Lulu.

“Nitakachokifanya nitamchukua hadi kijijini kwetu ambapo tutamlisha dawa ya kimila ambayo itatupa ukweli kama hiyo mimba ni ya Kanumba au mtu mwingine, hata kama…

Stori: Shakoor Jongo

BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kusekwa ameufungia kazi ujauzito wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuibuka na kueleza mkakati utakaomuwezesha kuikomboa damu ya mwanaye.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juzi, mzee huyo alisema yeye kama baba wa marehemu Kanumba, endapo maelezo ya kwamba Lulu ana ujauzito wa mwanaye yatafikishwa kwake, hawezi ‘kuchomoa’ ila atatumia dawa za kimila ‘DNA ya Kisukuma’ kubaini ukweli.
“Unajua hili suala la ujauzito wa Lulu linazidi kukua kila kukicha sasa mimi nitamaliza ubishi endapo nitakabidhiwa huyo Lulu.
“Nitakachokifanya nitamchukua hadi kijijini kwetu ambapo tutamlisha dawa ya kimila ambayo itatupa ukweli kama hiyo mimba ni ya Kanumba au mtu mwingine, hata kama kaitoa, dawa hiyo itaonesha,” alisema mzee Charles.
Akaongeza kuwa, hata hao wanawake wengine wanaodai kuzaa na mwanaye wamefanya makosa kwenda kumuona mama Kanumba kwani yeye hawezi kujua mambo ya mila za Kisukuma.
“Yule mama Kanumba hawezi kujua mila zetu, wangekuja kwangu wala nisingewakatalia ila ningewapa dawa ambayo naweza kumpa Lulu na ukweli ukajulikana,” alisema.
Lulu ambaye kwa sasa yuko katika Gereza la Segerea jijini Dar akikabiliwa na kesi ya kuhusishwa na kifo cha Kunumba, anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitatu huku ukitajwa kuwa ni wa marehemu Kanumba.
Chanzo:www.globalpublishers.info

NEC YATEUA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA


NEC YATEUA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana tarehe 12/5/2012 chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mambo mengine imefanya uteuzi wa Makatibu wa CCM wa Wilaya kama ifuatavyo:-

(1) Ndugu Grayson Mwengu
(2) Ndugu Abdallah M. Hassan
(3) Ndugu Ernest Makunga
(4) Ndugu Mgeni Haji
(5) Ndugu Innocent Nanzabar
(6) Ndugu Nicholaus Malema
(7) Ndugu Mercy Moleli
(8) Ndugu Michael Bundala
(9) Ndugu Elisante G. Kimaro
(10) Ndugu Zacharia Mwansasu
(11) Ndugu Eliud Semauye
(12) Ndugu Habas Mwijuki
(13) Ndugu Loth Ole Nesele
(14) Ndugu Charles Sangura
(15) Ndugu Donald Magessa
(16) Ndugu Fredrick Sabuni
(17) Ndugu Janeth Mashele
(18) Ndugu Daniel Porokwa
(19) Ndugu Zongo Lobe Zongo
(20) Ndugu Mwanamvua Killo
(21) Ndugu Joyce Mmasi
(22) Ndugu Simon Yaawo
(23) Ndugu Epimack Makuya
(24) Ndugu Amina Kinyongoto
(25) Ndugu Asia S. Mohammed
(26) Ndugu Venosa Mjema
(27) Ndugu Augustine Minja
(28) Ndugu Elly H. Minja
(29) Ndugu Ernest Machunda
(30) Ndugu Selemani Majilanga
(31) Ndugu Christina Gukwi
(32) Ndugu Joel Kafuge Mwakila
Vituo vyao vya kazi watapangiwa baadaye.

Mama Kikwete awataka wanawake kutokutoa mimba


Mama Kikwete awataka wanawake kutokutoa mimba

Na Anna Nkinda – Maelezo, Mbeya
Wanawake nchini wametakiwa kutokuwatupa watoto wanaowazaa hata kama wanakabiliwa na changamoto za kimaisha za kushindwa kuwalea kwani kwa kufanya hivyo wanamkosea Mwenyezi Mungu pia hawawezi jua watoto hao watakuwa na hali gani ya kimaisha kwa siku za baadaye.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake waliohudhuria sherehe za siku ya mwanamke wa Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo jijini Mbeya.
Aidha Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa usawa wa kijinsia katika elimu na fursa za kiuchumi zimeendelea kuwa changamoto kwa wanawake Duniani kote hata hivyo hatua kubwa imefikiwa ya kuwakomboa wanawake wengi kutoka lindi la umasikini.
“Tunatambua kwamba wanawake wanaposhiriki kikamilifu katika shughuli za jamii uchumi wa nchi hukua zaidi. Hivyo siku kama ya leo ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wanawake kujifunza kutoka kwa wengine jinsi walivyofanikiwa , kubadilishana uzoefu na kuelimishana. Kwani elimu yenye manufaa ni ile inayolenga kuwakomboa watu kutokana na changamoto zinazowakabili”, alisema Mama Kikwete.

Mhe. Lowassa awatuliza wanaCCM wasihamie Chadema


Mhe. Lowassa awatuliza wanaCCM wasihamie Chadema

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amekuwa na mikutano ya ndani katika jimbo lake katika kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za kutuliza wimbi la wana CCM kuhamia Chadema.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanaCCM katika mikoa mbalimbali kuhamia Chadema. Mkoa wa Arusha ndiyo unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa CCM wanaojiunga na Chadema.
Jana Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, alifanya mkutano wa ndani katika eneo la Mto wa Mbu na baadaye kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo wa hadhara, mbunge huyo aliwaambia wananachi kuwa pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya mtu, lakini haoni umuhimu wa wana CCM kwa sasa kuhama chama hicho kinachotawala.

Alisema CCM ni chama chenye kutetea maslahi ya wanyonge na kwamba kuna haja kwa wananchi kutathimini ili kuona kama kweli CCM imeshindwa kutimiza malengo yake.

Alisema CCM imekuwa ikitekeleza kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Jiulius Nyerere ambao nni umoja na mshikamano, vinavyoifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
Lowassa pia alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi na rasilimali za nchi ili zisiporwe na wageni.

Amewakumbusha kuwa CCM ni chama kinachotoa nafasi kwa wanachama wake kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila ya mizengwe au ubaguzi wa rangi, ukabila au dini.