MHE. JANUARY MAKAMBA AWATOA WASIWASI WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA


maka1

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akimpa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba jana 22/9/2016.

maka2

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akiwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba jana 22/9/2016.

maka4

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kulia) akimpa pole Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Ihunga Bw.Thomas Bonevanture mara alipowasili shuleni hapo kuwapa pole waathirika jana 22/9/2016.

maka5

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo kwenda kuangalia maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi jana 22/9/2016 Wilayani Misenyi.

maka6

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakiwapa pole baadhi ya waathirika wa tetemeko la ardhi Wilayani Misenyi leo 22/9/2016.

Na Benedict Liwenga-WHUSM, Bukoba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba amewatoa wasiwasi waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Wilayani Bukoba Mkoani wa Kagera.

Mhe. Makamba ameyasema hayo leo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa lengo la kuwapa pole waathirika na kuwap ujumbe wa Serikali kuhusu namna inavyojitahidi kuwasaidia waathirika hao.

Amesema kwamba, wananchi wasiwe na wasi wasi kuhusu suala la kupatiwa misaada ya dharura kwani Serikali imejipanga na bado inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea ingawa zoezi la kuwapatia baadhi ya huduma za msingi linaendele.

“Tumekuja kutoa msaada kwa mji kwa ujumla wakati tunapanga namna ya kusaidia katika masuala ya mazingira na tambueni kuwa Serikali inawajali ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wako hapa na wengine wanazidi kuja”, alisema Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa, suala la kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo limepewa uzito mkubwa na Serikali na suala la kuchelewa kwa kutolewa kwa misaada kunatokana na umakini unaoendelea kufanywa sasa hivi na Serikali ili kuwatendea haki waathirika pekee.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.

Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika hao.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa na amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.

Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

MBUNGE WA SIMANJIRO JAMES OLE MILYA AZINDUA MADARASA MANNE YA SHULE YA MSINGI EMBOREET MARA,SIMANJIRO


Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akishikana mikono na  Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter ishara ya  uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.Picha na Woinde Shizza

Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Emboreet mara baada ya kuzindua madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.

Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akiteta jambo na Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter katika uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.PICHA NA WOINDE SHIZZA

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU.

Mkutano wa Kilele wa G20 waanza China


Mkutano wa kilele wa siku mbili wa kundi la G20 umefunguliwa nchini China Jumapiliv (04.09.2016) kwa wito kwa chombo hicho kuwa timu ya vitendo badala ya kuwa mahala pa kupiga porojo.

Akifunguwa mkutano huo katika mji wa Hangzhou Rais Xi Jinping wa China amesema anataraji huko Hangzhou wanaweza kushughulikia dalili za matatizo halikadhalika sababu kuu za matatizo ya uchumi wa dunia …..”G20 inapaswa ibadili mtizamo wake na kuweka umuhimu sawa kwa sera za muda mfupi na sera za muda mrefu.”

China ni mwenyeji wa viongozi 20 wa kundi hilo la nchi zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi duniani na zile zenye kuinukia kiuchumi katika mji mashuhuri wa kihistoria wa Hangzhou ulioko mashariki mwa China kuanzia Jumapili (04.09.2016) hadi Jumatatu ambapo usalama umeimarishwa kwa kuwekwa kwa vikwazo barabarani.

Rasi Xi alisalimiana kwa kupeana mikono na wageni waliokuwa wakiingia mmoja baada ya mwengine katika kituo cha Maonyesho ya Kibiashara cha Kimataifa cha Hangzhou kunakofanyika mkutano huo miongoni mwao Rais Barack Obama wa Marekani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Rais Vladimir Putin wa Urusi, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Dhima ya China

Tukio hilo linaonyesha dhima ya China katika jukwaa la dunia wakati baadhi ya viongozi wakitarajiwa kuishinikiza China kutii kanuni za kimataifa za biashara na uzaslihaji wake wa kupindukia wa chuma.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Xi amesema kundi hilo la G20 halipaswi kuchukuwa hatua mpya za kuhami masoko na badala yake ichukuwe hatua madhubuti za kuchochea ukuaji wa uchumi duniani.

Obama na XI walikutana Jumamosi jioni ambapo nchi zote mbili zilitangaza kujiunga rasmi na makubaliano ya Paris ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati wa mazungumzo yao yaliochukuwa muda mrefu Xi aliihimiza Marekani kutimiza dhima yenye tija katika kudumisha amani na utulivu katika eneo la Bahari ya China Kusini.China inadai kumiliki takriban eneo lote hilo ambalo pia linagombaniwa na Vietnam, Taiwan,Ufilipino,Malaysia na Brunei.

Nafasi ya vyombo vya habari yaleta tafrani

Mkutano wa Xi na Obama ulitiwa kiwingu na mzozo kuhusu suala la vyombo vya habari kuuangazia mkutano huo ambapo hapo Jumapili Rais Obama alikiri kwamba kulikuwepo na mvutano kuhusiana na sisitizo la Marekani la kujumuishwa kwa vyombo vya habari wakati wa Mkutano huo wa kilele wa kundi la mataifa 20 ambapo amesema hatoomba radhi kwa kuvitetea vyombo vya habari.

Akizungumza katika mkutano huo Obama amesema “tunafikiri ni muhimu kwamba vyombo vya habari vinapatiwa nafasi ya kuelewa kazi tunayoifanya ili wawe na uwezo wa kujibu maswali. Hatuyaachi nyuma maadili yetu wakati tunapofanya safari hizi.”

Mzozo huo ulianza mara baada ya kutuwa kwa ndege ya Air Force One katika mji wa Hangzhou hapo Jumamosi ambapo kundi la waandishi wa Kimarekani lililokuwa likiandamana na Rais Obama lilipozuiliwa wakati rais alipokuwa akiteremka kwenye ndege ambapo afisa wa China aliwapigia makelele wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani kuwaondowa kabisa waandishi wa habari katika eneo hilo.

Wakati afisa wa Ikulu aliposema hilo lilikuwa ni suala linamhusu rais wa Marekani na kwamba hiyo ilikuwa ni ndege ya Marekani kwa hiyo waandishi hao wataendelea kubakia katika eneo hilo afisa huyo wa China alijibu kwa ukali kwamba “Hii ni nchi yetu”.

Afisa huyo pia alipapurana na Mshauri wa Usalama wa Taifa Susan Rice na Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa Ben Rhodes wakati walipokuwa wakijaribu kutembea karibu na Rais Obama.Kuhusiana na kisa hicho Rice alisema baadae “Wamefanya mambo ambayo hawakuyategemea.”

Mvutano huo uliendelea tena hapo Jumapili wakati sehemu ya mkururo wa vyombo vya habari uliokuwa ukimsindikiza Obama ulipozuiliwa kukaribia eneo la mapokezi la mkutano huo wa kilele wa G20.

Mbali na suala la ukuaji wa uchumi mkutano huo unatowa fursa kwa viongozi kujadili masuala mbali mbali muhimu duniani.DW

SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA MATUKIO YA MOTO MKOANI ARUSHA


A1

Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sarah Mlaki, akimkabidhi cheti cha kumaliza darasa la saba mhitimu Mercygracious Tolla wa Shule ya Msingi ya Macedonia kwenye mahafali ya tano ya shule hiyo iliyoko Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.

A2

Hussein Makame-MAELEZO

SERIKALI imesema itawachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kwa sababu moja au nyingine kuhusika na matukio ya moto yaliyotokea mkoani Arusha hivi karibuni.

Hayo yamesema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. SimonMsanjila katika mahafali ya tano ya Shule ya Msingi ya Macedonia iliyopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza kwa niaba ya Prof. Msanjila ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi wa wizara hiyo Sarah Mlaki alikuwa akijibu kilio cha Mkuu wa shule hiyo aliyelaani matukio hayo ya moto kuendelea kujitokeza huko mkoani Arusha na maeneo mengine.

Alisema mbali na kuwachukulia hatua wahusika, Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni nchini.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni.Tutachukua hatua stahiki kwa wale ambao watabainika kwa sababu moja au nyingine wanahusika na majanga hayo”, alisema Mkurugenzi Mlaki.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Serikali pia imejipanga kuboresha miundombinu ya shule zake ili watoto Watanzania wapate haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mlaki alisema soko la vitabu vya kiada vinavyotumika katika shule  za msingi nchini limevamiwa na watu mbalimbali na Serikali inafahamu kuwa kuna vitabu vingine havina ubora unaostahili kwa matumizi ya shule.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mlaki alisema Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada ili wanafunzi wote kutumie vitabu hivyo bila ya kuwa na tofauti katika elimu inayotolewa.

“Kwa kweli soko la vitabu limevamiwa na watu mbalimbali na tunafahamu kuna vitabu vingine havina ubora stahiki, lakini Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada (text book) ili wanafunzi wote waweze kutumia vitabu hivi pasiwe na tofauti katika elimu inayotolewa” alisema Mkurugenzi Mlaki.

Aliongeza kuwa anaamini kwamba tatiz hilo litatatuliwa kadri siku zinavyokwenda kwa kuwa taasisi husika tayari inalishughulikia suala hilo kulingana na uzito wake.

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 53 wa shule hiyo walihitimu na wanatarajia kufanya mitihani ya taifa ya darasa la saba mwaka huu, wakiwemo wanafunzi 24 wanaume na wanawake 29.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Shukuru Mbwire alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009, imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na la nne ambapo ilianza na wanafunzi 70 lakini hadi sasa ina wafanuzi 782.

Alisema katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la saba shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka ambapo katika mitihani ya mwaka 2015 shule hiyo ilipata wastani wa daraja A na kushika nafasi ya 3 kati ya shule 56 kiwilaya, nafasi ya 28 kati ya shule 534 kimkoa na kitaifa ilishika nafasi ya 219 kati ya shule 16,096.

“Kwa miaka yote hiyo shule ilifaulisha wanafunzi kwa asilimia 100 ambapo watoto wote walifanikiwa kujiunga na shule za Sekondari za vipaji maalum na zile za kawaida” alisema Mbwire.

Katika risala ya wanafunzi wa shule hiyo, wahitimu walitangaza kumuunga mkono kaulimbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu na kuwataka Watanzania wafanye kazi kwa bidii ili kulikomboa Taifa na umasikini.Chanzo:mjengwablog

ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA-MAJALIWA


 

H1

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watalaam na wajenzi wa Chuo wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

H2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa kuhusu  ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kwa  Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Ephata Kaaya wakati alipokagua ujenzi huo  eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016. Kulia  kwake ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

H3

H4

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ufungaji vifaa vya tiba wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa  Chuo wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016. Kushoto  kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa, Ephata Kaaya.

H5

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama mashine ya CT Scanner wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa  Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016.

H6

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa  Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016.

H7

 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua jiko wakati alipolea eneo ilipojengwa  Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam  Septemba  2, 2016. Watatu kushoto  ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Ephata Kaaya. 

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha wataalam hao nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 2, 2016) wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila.

Amesema Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.

“Wafanyakazi waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,” amesisitiza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.

Amesema hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ujenzi wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha  chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.

Prof.  Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.

 IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

  1. L. P. 3021,

11410 DAR ES SALAAM. 

IJUMAA, SEPTEMBA 2, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA RIPOTI YA HALI YA HEWA BARANI AFRICA


 

1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na  Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya  Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa  katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye  hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.

2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na   Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya  Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye  hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.

3

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kutoka kwa Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa  wa   Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa,  Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye  hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.

4

Picha ya pamoja.

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)