Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Ashiriki Mazishi Ya Aliyekua Mnikulu katika Ikulu ya Zanzibar,Marehemu Shaaban Ahmada Hilika


Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Ashiriki Mazishi Ya Aliyekua Mnikulu katika Ikulu ya Zanzibar,Marehemu Shaaban Ahmada Hilika

Shekh.Talib Suleiman, akisoma dua baada ya kumaliza kuzika katika makaburi ya Vuga Mkadini Unguja.

Advertisements

Daily Word Salutes “Whoa”-Inspiring Women: Define Yourself!!!


Daily Word Salutes “Whoa”-Inspiring Women: Define Yourself!!!

Happy Tuesday, my Great ones!

Welcome to day two of our special celebration of women who have inspired us to be great! Today’s Daily Word is dedicated to Defining Yourself… and who better to represent this topic than Ms. Dana Owens or Queen Latifah as we better know her as. From her introduction into the world, she has always marched to her own beat! Ms. Owens burst onto the scene defying everything that she was told wouldn’t work, and she rewrote the rules to work in her favor – from dominating a man-driven music genre, to redefining what society called beauty.

She has won Golden Globes, Image Awards, and Grammys, Has been nominated for Emmys and Oscars, starred in Musicals, and Hollywood blockbusters alongside A-List actors such as Catherine Zeta-Jones, Steve Martin, Diane Keaton, and Dolly Parton. She is a celebrity spokesperson for Covergirl cosmetics, Curvation ladies underwear, Pizza Hut, and Jenny Craig, and has her own line of cosmetics for women of color called the CoverGirl Queen Collection. Transitioned from Hip-Hop into Jazz and R&B, singing alongside great talents such as Jill Scott, Erykah Badu, and Stevie Wonder. Sung “America the Beautiful” at the 2010 Super Bowl, owns her
own movie production company which releases both theatrical and straight to DVD releases…

Ohh….and did I mention that she started as a rapper from the rough streets of Newark, New Jersey? The point is that, from her inception, Ms. Owens was being told what she could and could not do, but instead of allowing others to set limitations on her, she took her life in her own hands and defined for herself what was possible! Greatness is simply that – the ability to take your life in
your own hands and give your best in whatever you do! For that, Ms. Dana Elaine Owens, we Salute you!! All Hail the Queen!!!
-Ash’Cash

“We must not allow other people’s limited perceptions to define us.” -Virginia Satir

“Be a first rate version of yourself, not a second rate version of someone else.” -Judy Garland

“Life is not what it’s supposed to be. Its what it is. The way you cope with it is what makes the difference.” -Virginia Satir

“When it is obvious that the goals cannot be reached, don’t adjust the goals, adjust the action steps.” -Confucius

“Your mistake does not define who you are…you are your possibilities.” -Oprah Winfrey

“Be who you are and say what you feel because those who mind don’t matter and those who matter don’t mind.” -Dr. Seuss

“Life isn’t about finding yourself. Life is about creating yourself.” -George Bernard Shaw

“Do not go where the path may lead; go instead where there is no path and leave a trail.” -Ralph Waldo Emerson

TO HEAR THE AUDIO VERSION OF THE DAILY WORD – CLICK HERE.

Ash’Cash is a Business Consultant, Motivational Speaker, Financial Expert and the author of Mind Right, Money Right: 10 Laws of Financial Freedom. For more information, please visit his website, http://www.IamAshCash.com.Chanzo:www.allhiphop.com

Miundombinu ya Tanesco ‘imechoka’


Miundombinu ya Tanesco 'imechoka’


Zaina Malongo

WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu.

Kauli hiyo imekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya vyombo vya habari, kutangaza kuwepo kwa mgao wa umeme nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, alisema mgao ulijitokeza za katika Mkoa wa Dar es Salaam, ulisababishwa na kuungua kwa transfoma mbili zenye ukubwa wa 15 MVA na Kv 33/11 zilizopo katikati ya Jiji.

Alisema tatizo hilo lilianza Machi 6 mwaka huu ambapo umeme ulikatika kutokana na hitilafu katika kituo cha kupoozea umeme ilichoko mkabala na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Maswi alisema baada ya hitilafu hiyo, Serikali iliamua kugharamia manunuzi ya ya transfoma nne zenye thamani ya Dola 350 milioni kwa utaratibu wa dharura.

Kuhusu deni la Tanesco la Sh 279 bilioni, alisema deni hilo si la kweli na kwamba deni halisi ni Sh 79 bilion.

“Deni tunalodaiwa ni Sh 79 bilioni lakini wao wamejulisha hadi madeni ya miradi ambayo imeingia mikataba na shirika pamoja na makampuni ambazo zinafanya kazi na shirika letu,”alisema na kuongeza

Katika hatua nyingine, wizara ipo katika mkakati wa kuongeza megawati 100 za umeme ili kufikia megawati 1370

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando, alisema baada ya kupata Sh 408 bilioni shirika linajipanga kubadilisha miundombinu yake.Chanzo:mwananchi

KABURU AZIKA MGOMO WA WACHEZAJI SIMBA SC


KABURU AZIKA MGOMO WA WACHEZAJI SIMBA SC

Na Dina Ismail
WAKATI mgomo baridi miongoni mwa wachezaji wa Simba ukipatiwa ufumbuzi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuokoa jahazi, uongozi wa klabu hiyo umemtema katika safari ya Algeria kiungo wake wa kimataifa, Patrick Mutesa Mafisango.
Wachezaji wa Simba waliendesha mgomo wa chini chini kwa karibu siku tatu, wakishinikiza walipwe sh mil. 30 walizoahidiwa na uongozi – iwapo wangeifunga ES Setif ya Algeria, waliyocheza nayo Jumapili iliyopita katika mechi ya awali raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho (CAF) kwenye Uwanja wa Taifa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuambulia sh milioni 15 tu.
Habari kutoka katika kambi ya klabu hiyo iliyoko Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa Kaburu alikwenda kambini na kuwaongeza shilingi milioni tano na hivyo kuamua kuachana na mgomo huo.
Imeelezwa kuwa pamoja na mgao huo, kulifanyika kikao juzi jioni ambapo wachezaji waliamua kuuzika mgomo huo na kujipanga kikamilifu tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzanuia Bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa kesho katika dimba la Taifa Dar es Salaam na ile ya marudiano dhidi ya ES Setif itakayopigwa wiki mbili zijazo.
Aidha suala hilo la kudai malipo hayo pia lilipelekea Mafisango kusimamishwa, baada ya kurejea kambini akiwa amelewa na kuanza kumtolea lugha chafu Meneja wa Timu hiyo, Nico Nyagawa, kabla ya kutaka kumpiga Kocha Mkuu, Mserbia Milovan Cirkovic, yote ikiwa ni katika kudai maslahi ya timu hiyo.
Habari zinadai kuwa katika vurumai hiyo, Mafisango aliulalamikia uongozi wa Simba kutojali maslahi ya wachezaji, huku akimshutumu Nyagawa kwa kushindwa kuwatetea pindi walipotaka waongezewe mgao wao. Hata hivyo Mafisango alikuwa hajajua kama tayari wameshaongezwa milioni tano.
Tayari uongozi wa Simba umempa barua ya kumsimamisha kuichezea timu hiyo kwa muda, sambamba na kumtaka ajieleze kutokana na kufanya utovu wa nidhamu kwa waajiriwa wengine wa klabu hiyo katika kambi ya timu hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga ilisema kuwa kutokana na utovu huo wa nidhamu, Mafisango hatasafiri na timu kwenda Algeria wiki ijayo itakapoenda kukwaana na Setif ya huko katika mchezo wa marudiano.
“Uongozi tayari umemuandikia barua ya kutaka ajieleze kwa makosa yake na maamuzi kamili yatatolewa mara timu itakaporejea kutoka Algiers,” ilieleza taarifa hiyo.

Rebecca Malope kuwasili nchini Aprili 6 akitokea Afrika Kusini


Rebecca Malope kuwasili nchini Aprili 6 akitokea Afrika Kusini

Na Mwandishi Wetu

MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, anatarajia kuwasili nchini Aprili 6 mwaka huu, ili kutumbuiza katika tamasha la nyimbo za Injili la Pasaka litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Alex Msama, alisema Rebecca anatarajia kuwasili na kundi la wanamuziki wake 13.

“Rebecca ameahidi atapiga ‘live’ akishambulia jukwaa kwa takriban saa 2 na ushei na atapiga nyimbo zake mpya tano na nyingine za zamani,” alisema Msama.

Akizungumza kwa njia ya simu wiki hii kutoka Afrika Kusini, Rebecca aliahidi kuwaletea Watanzania zawadi ya Pasaka, na akabainisha ataambatana pia na waimbaji wengine kutoka Afrika Kusini.

Rebecca alisema amewaandalia zawadi nzuri mashabiki wa muziki wa Injili wa Tanzania, na akatoa mwito wajitokeze kwa wingi siku ya tukio ili kumshuhudia.

“Naahidi kuwaletea Watanzania zawadi ya Pasaka… nimewaandalia vitu vipya ambavyo naamini watavifurahia,” alisema Rebecca.

Rebecca aliyezaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini, alisema katika tamasha hilo la Pasaka mwaka huu ataimba nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake, zikiwemo tano mpya.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

Malope atakuwa mmoja kati waimbaji siku hiyo wakiwemo Rose Muhando, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu ambako mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika, Job Ndugai.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.