Zitto Kabwe:Dr.Ulimboka Kutekwa,Kupigwa Na Kuumizwa Serikali Inawajibika Kutueleza


Advertisements

MZEE KUSEKWA: MAMA KANUMBA AACHE UJANJA


Stori: George Kayala

SIKU chache baada ya habari kuwa mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kutoka gazetini kuwa amenunua nyumba, mzazi mwenzake mzee Charles Kusekwa ameibuka na kumtaka aache ujanjaujanja.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea Shinyanga, mzee Kusekwa alisema mama Kanumba hana fedha ya kununua hiyo nyumba ya mamilioni iliyopo Kimara – Temboni, Dar.

HII HAPA SAUTI YAKE

“Unajua mwenzangu anataka kudanganya watu, anajifanya amenunua hiyo nyumba ili iwe yake na isiingie kwenye mirathi. Anaweza kuwadanganya wasioelewa lakini mimi nasema hana pesa ya kununua nyumba.

“Aache ujanjaujanja, hiyo ni nyumba ya Kanumba na inatakiwa iingie kwenye orodha ya mirathi. Anunue nyumba kwa pesa gani aliyonayo?”

MAMA KANUMBA…

Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.

Mzee Charles Kusekwa.

Stori: George Kayala

SIKU chache baada ya habari kuwa mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kutoka gazetini kuwa amenunua nyumba, mzazi mwenzake mzee Charles Kusekwa ameibuka na kumtaka aache ujanjaujanja.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea Shinyanga, mzee Kusekwa alisema mama Kanumba hana fedha ya kununua hiyo nyumba ya mamilioni iliyopo Kimara – Temboni, Dar.

HII HAPA SAUTI YAKE
“Unajua mwenzangu anataka kudanganya watu, anajifanya amenunua hiyo nyumba ili iwe yake na isiingie kwenye mirathi. Anaweza kuwadanganya wasioelewa lakini mimi nasema hana pesa ya kununua nyumba.
“Aache ujanjaujanja, hiyo ni nyumba ya Kanumba na inatakiwa iingie kwenye orodha ya mirathi. Anunue nyumba kwa pesa gani aliyonayo?”

MAMA KANUMBA NAYE
Juhudi za kumpata mama Kanumba kwa njia ya simu ziligonga mwamba, lakini mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco alipopatikana alitoa ushirikiano.

TUJIUNGE NA SETH BOSCO
“Mzee anapotosha, nyumba imenunuliwa mbele ya mwanasheria na vielelezo vyote vipo. Kama ataleta kipingamizi chochote, atakutana na nyaraka zote halali.”

TUJIKUMBUSHE
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu mali za marehemu Steven Kanumba, ambapo wawili hao kila mmoja amekuwa akivutia upande wake.
Ilifikia mahali mzee Kusekwa alituma wawakilishi wake katika Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni kwa lengo la kufungua mirathi, lakini aligonga mwamba kwa kukosa hati ya kuzaliwa na kifo cha marehemu.

Chanzo:www.globalpublishers.info

 

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Afungua Semina ya Siku mbili Kuhusu Kuimarisha Uhusiano Baina ya Wanasiasa na Watendaji Katika Serikali za Mitaa Zanziba


 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua semina ya siku mbili kuhusu kuimarisha Uhusiano Baina ya Wanasiasa na Watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,alipowasili katika viwanja vya Zanzibar Beach Resort,alipohudhuria katika semina ya siku mbili ya Uongozi ya Viongozi  wa Serikali za Mitaa Zanzibar,akiwa ni Mwenyekiti wa Semina hiyo iliyoanza Leo.
Sheha wa Shehia ya Ubago,Wilaya ya Kati Unguja,Mkoa wa Kusini Unguja,Bibi Asha Abeid Suba,akichagia suala la Maji wakati wa Semina ya siku mbili,juu ya Kuimarisha Uhusino baina ya Wanasiasa na Watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,iliyoanza leo katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja.
 
 Baadhi ya Madiwani na Masheha wa Shehia mbali mbali za Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba ya ufunguzi wa semina ya siku mbili juu ya Kuimarisha Uhusiano baina ya Wanasiasa na Watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,iliyoanza leo, katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,Nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame,alipowasili katika viwanja vya Zanzibar Beach Resort,alipohudhuria katika semina ya siku mbili ya kuimarisha Uhusiano baina ya Wanasiasa na Watendaji wa Serikali za Mitaa Zanzibar,akiwa Mwenyekiti wa Semina hiyo iliyoanza Leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.-Zanzibar

Simba Awataka Waislamu Kushiriki Sensa.


 

SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba ametoa msimamo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
 
Kauli hiyo ya Mufti Simba inakuja siku chache baada ya tamko la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania likiwataka Waislamu wote kutoshiriki kwa shughuli hiyo kwa kile walichodai ni kutoingizwa kipengele cha dini kwenye dodoso la Sensa.
 
Hii ni mara ya pili kwa Mufti Simba kuzungumzia suala hilo, mara ya kwanza ikiwa ni Juni 6, mwaka huu alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga na kuitaka Serikali kuingiza kipengele cha dini katika dodoso la Sensa.
 
Alisema kalenda iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa takwimu zinazoonyesha idadi ya Watanzania ni 43 milioni, kati yao wakristo ni asilimia 52, waislamu asilimia 32 na dini nyingine wako asilimia 16.
 
Mufti Simba alipinga na kulaani takwimu hizo kwamba si sahihi na zinapotosha wananchi, kwa sababu Sensa iliyofanyika mwaka 2002 haikuhusisha kipengele kinachobainisha dini za Watanzania.
 
“Kwa kuwa taarifa hizi zinaonekana kwenye kalenda ya waziri mkuu, tunaitaka Serikali kurudisha kipengele kinachobainisha dini za Watanzania mwaka huu ili ukweli ubainike kwa lengo la kuondoa kabisa sintofahamu hiyo,” alisema Mufti Simba.
 
Lakini, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mufti Simba alisema walichokuwa wakipinga Waislamu ni baadhi ya watu kuanza kutoa takwimu za idadi ya Wakristo na Waislam wakati hawana dhamana na mamlaka ya kufanya hivyo.
 
Akisisitiza umuhimu wa Waislam kujitokeza kuhesabiwa, Mufti Simba alisema, “Mimi kama kiongozi wa Waislamu natoa wito kwa Waislamu wote hapa nchini, kushiriki kwa ukamilifu katika zoezi la Sensa litakalofanyika nchini mwetu.”
 
Aliongeza: “Katika nchi yetu Sensa zimefanyika nyingi miaka ya nyuma na hazikuhusishwa na dini wala ukabila, ni jambo lililo zoeleka na kukubalika.”
Mufti Simba alisema kilichojitokeza hivi karibuni ni takwimu za Sensa kutolewa na watu ambao hawana dhamana hiyo, na Serikali inatakiwa kutunga sheria itakayomuainisha atakaye kuwa na dhamana ya kutoa taarifa hizo.
 
“Waislamu wasisite kuiomba Serikali iwafafanulie takwimu za Sensa ambazo zilikuwa zikitolewa kuwa Waislamu wako kadhaa, na Wakristo wako kadhaa, kama serikali inazitambua takwimu hizo,” alisema Mufti Simba na kuongeza:
 
“Katika tovuti mbalimbali na hata za Serikali kuna taarifa kuwa Waislamu wako takriban asilimia 35. Sasa hizi hatujui zimepatikana wapi na nani amezitoa.”
Mufti Simba alisema kilichowakera Waislamu si nafasi ya Sensa, kwa sababu Sensa ina lengo, ni jambo la kisheria na ni la kimaendeleo katika nchi.
 
Hata hivyo, katika mkutano huo na waandishi wa habari Mufti Simba hakutoa nafasi ya kuulizwa maswali, baada ya kusoma tamko lake la aya sita aliondoka na kuwaacha waandishi wakishangaa kwa nini imekuwa hivyo.
 
Tamko la Jumuiya
Wiki iliyopita Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema baada ya Serikali kukataa mapendekezo matatu waliyowasilisha, walikubaliana kutoshiriki Sensa na wataifikisha Serikali mahakamani.
 
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuitaka Serikali kushauriana na wawakilishi wa dini, iunde tume huru ya Sensa na kuitangaza kabla ya Agosti 20, mwaka huu, tume hiyo iwe na wawakilishi wa madhehebu ya Waislamu, Wakristo na mengine katika hatua zote za mchakato huo. 

MSANII WA FILAMU ELIZABETH MICHAEL (LULU)ALIPOFIKISHWA MAHAKAMANI


 Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akipanda basi la Magereza huku akijaribu kukwepa kamera za waandishi wa habari jana mara baada ya kutoka kusikiliza kesi ya kudaiwa  kuuwa inayomkabili kwenye Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam baada ya kesi hiyo kuhairishwa hadi 9.7.2012. 
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Lulu akielekea kupanda kwenye basi  tayari kuelekea magereza katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi Ahimiza Vijana ndani ya CCM na Jumuiya Zake Kuendelea Kutunza Amani iliyopo na Kujiepusha na Shari inayoweza Kuzaa Balaa


 
  Mjumbe wa kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha Suleiman Iddi akisisitiza jambo wakati akiufungua Mkutano wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya hiyo hapo Ukumbi wa CCM Jimbo la Kitope uliopo Kinduni.
  Mjumbe wa Kamati wa Siasa ya CCM Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi mchango wa shilingi Laki Tatu { 300,000/- } Mwenyekiti wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Wilaya ya Kaskazini B nd. Mosi Ame Mosi. Mchango huo ni kwa ajili ya kusaidia utunishaji wa mfuko wa Umoja huo ambao ni muhimili muhimu katika uhamasishaji ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Wajumbe wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya ya Kaskazini “B” wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wao iliyotolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani. Ufunguzi huo umefanyika katika Ofisi ya CCM ya Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini B. 
 Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wamesisitizwa kuendelea kutunza amani iliyopo na kujiepuka na shari inayoweza kuzaa balaa na hatimae kuzagaa kwa maafa Nchini. 
 
Sisitizo hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Kaskazini B ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wapanda Mapiki Pili wa Wilaya hiyo hapo Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope uliopo Kinduni. 
 
Mama Asha amesema Vijana hao wanapaswa kuwa waangalifu zaidi kutokana na vitendo vinavyoashiria fujo ambavyo huonekana kukumba zaidi kundi kubwa la Vijana.
 
 Amesema suala la utunzaji wa Amani linamuhusu kila Mwana Jamii kwani hata Dini zote pamoja na Madhehebu mbali mbali zimekuwa zikihubiri na kuhimiza suala la utunzwaji wa Amani. 
 
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mama Asha aliwahimiza Wajumbe wa Mkutano huo kuhakikisha Wanawachaguwa Viongozi Makini watakaokuwa Mahiri kwenye uendelezaji wa Ushindi wa Chama chao Katika Uchaguzi ujao. 
 
Alisema Tabia ya Baadhi ya Watu kuchagua Viongozi kwa misingi ya Ukabila na kujuana imepelekea kukitia doa kubwa Chama Hicho ambacho ndio kimbilio la Wanyonge Nchini. “ Ukweli tabia hii mbaya sana inakera na inafaa kuepukwa mara moja kwa vile inapunguza kwa kiasi kikubwa nguvu ya Chama ”. Alisisitiza Mama Asha. 
 
Mama Asha aliwakumbusha Vijana hao kuendelea kuyatetea Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambayo yalileta faraja kwa Wananchi walio wengi hapa Zanzibar. Alisema Vijana wanapaswa kuwa makini katika kutetea Viongozi wao kutokana na tabia ya baadhi ya watu kuendeleza tabia ya kuhubiri Matusi hadharani hana sababu dhidi ya Viongozi hao. 
 
Katika kuunga Mkono juhudi za kuendeleza Umoja huo wa Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha amechangia jumla ya Shilingi Laki Tatu Taslimu { 300,000/- } kusaidia kutunisha Mfuko wa Umoja huo. 
 
Katika Risala yao iliyosomwa na Katibu Msaidizi wa Umoja huo Nd. Ame Pandu Kombo Vijana hao wameahidi kuendelea kuhamasisha Wananchi pamoja na Wanachama katika kuunga mkono Sera za Chama Tawala ambacho ndio kimbilio la Wananchi walio wengi Nchini. Nd. Ame alisema Umoja wao licha ya kazi kubwa wanayoendelea kuitekeleza lakini bado wanakabiliwa na Changa moto mbali mbali zinazokwamisha kutekeleza majukumu yao. 
 
Alizitaja Changa moto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa sare wakati wanapokuwa katika shughuli zao za uhamasishajipamoja na Mtaji mdogo wa Umoja wao unaopelekea kushindwa pia kufungua Akaunti Benki. 
 
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Wilaya ya Kaskazini B Nd. Mosi Ame Mosi aliwatahadharisha Vijana hao kuwa mbali na Makundi ya sasa yanayopandikizwa cheche za kuchafua amani ya Nchi katika maeneo mbali mbali hapa Nchini. 
 
 
  Na 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar

Musri wa Muslim Brotherhood mshindi


 
Mohamed Mursi
Mohammed Mursi ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa Rais nchini Misri.

Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.
Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.

Wafuasi washangilia Cairo

Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.

Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.