RAIS KIKWETE AFUTURISHA MKOANI LINDI …


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi leo Julai 30, 2012
 
Mkuu wa Mkoa a Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akishiriki katika futari hiyo pamoja na waalikwa wengine
Kadhi wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Shekhe Mkuu wa Mkoa Mohamed Saidi Mushangani akitoa neno la shukurani baada ya futari
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na waalikwa walioshiriki katika futari hiyo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa baada ya kufuturu

TAMKO LA TASWA KUHUSU CECAFA


CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya Baraza la Michezo la Vyama vya michezo la Afrika Mashariki (CECAFA),  kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari katika mchezo wa fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kufuatia kudhalilishwa huko kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya kombe la Kagame kati ya Yanga na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na kuwaondolea utu, udhalilishaji na unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi yao kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.

Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania wamekuwa wasikivu, waadilifu na watu wanaofuata taratibu,  lakini katika fainali hiyo mara baada ya mchezo walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.

Lengo la waandishi si kuleta vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa kila tukio lilikuwa linatokea uwanja, badala yake walionekana hawana thamani mbele ya jamii inayowawakilisha.

TASWA inalaani kitendo cha Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa agizo kwa polisi kuwazuia waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao za kuhoji makocha na wachezaji, hali iliyosababisha vurugu.

CECAFA walijenga urafiki wa karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano hayo na Kagame kwa lengo la kuyatangaza , lakini mwisho wa yote walionekana kama taulo la deki limekuwa na thamini pale ambapo linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani tena.

Lakini TASWA inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama baadhi ya viongozi wa TFF na CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kutoa maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye

Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo

1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).

2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote yaliyo chini ya  CECAFA.

Ili kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka kuombwa radhi na CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi ambao wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.

TASWA inatoa onyo kali kwa baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia ya kutotoa ushirikiano na dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi zao.

Juma Abbas Pinto

CHAIRMAN

Julai 30, 2012

 

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA ROTARY TANZANIA


 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rotary Tanzania na Rais wa Rotary Interantional 2012-13, Sakuji Tanaka, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam kwa mazungumzo jana Julai 28, 2012.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Rotary International 2012-13, Sakuji Tanaka, baada ya kumaliza mazungumzo wakati Rais huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam jana Julai 28, akiwa na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Rotary Tanzania, na Rais wa Rotary International 2012-13, Sakuji Tanaka, baada ya mazungumzo wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, jana Julai 28, 2012 kwa mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Nafasi Za Kazi TANAPA


 
Tanzania National Parks (TANAPA) is a Parastatal organization charged with legal mandate to manage and regulate the use of areas designated as National Parks so as to preserve the country’s heritage of natural and cultural resources in Tanzania. The mission of TANAPA is therefore to sustainably conserve and manage park resources and their aesthetic values for the benefit of present and future generations of mankind and provision of high class tourism products and services. In order to efficiently carry out this mission, TANAPA is seriously looking for highly qualified Tanzanians to fill the following vacancies:-

GEOGRAPHIC INFORMATION SYSTEM OFFICERS

ASSISTANT PARK ECOLOGISTS

ANIMAL HEALTH TECHNICIAN II

LABORATORY TECHNOLOGIST

TOURISM PROMOTION OFFICERS II

PRINCIPAL MARKETING OFFICERS

GRAPHIC DESIGNER II

ASSISTANT GRAPHIC DESIGNER

OFFICE SUPERVISOR

PRINCIPAL HUMAN RESOURCES AND ADMINISTRATIVE OFFICER

PARK RANGERS IV

RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II

HUMAN RESOURCES AND ADMINISTRATIVE OFFICER II

SENIOR HUMAN RESOURCE AND ADMINISTRATIVE OFFICER

MODE OF APPLICATION
Only qualified persons should submit their hand written letters of application with copies of relevant academic, school leaving and professional certificates, copy of Birth certificate and testimonials so as to reach the undersigned within 21 days from today 26/07/2012. Applicants are also required to indicate the names and contacts of at least two referees.

NB: Applicants are advised to keenly observed the stipulated job requirements as applications which do not relevantly meet the respective will not be considered.

DIRECTOR GENERAL,
TANZANIA NATIONA PARKS
P.O.BOX 3134
ARUSHA.
Te: 255 27 2503471/2501930 – 31
Fax: 255 27 2508216
Email:dg@tanzanianationalparks.com
TANAPA is an employer of equal opportunity

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akiwapongeza Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo Naibu Waziri Stephen Masele


 
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwapongeza Waziri wa Nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kushoto),NaibuWaziri wa Wazara hiyo, Stephen Masele (wapili kulia)  na  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Eliachim Maswi baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo Mjini Dodoma Julai 28,2012. Picha na Ofisi ya Waziri mkuu

RAIS WA ZANZIBAR AAGIZA KUNUNULIWA KWA MELI MPYA YA ABIRIA NA MIZIGO


 
 
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameagiza ndani ya wiki moja kuandaliwe utaratibu wa ununuzi wa meli ya abiria na mizingo yenye uwezo wa kubeba abiria 1000.
 
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jioni ya Julai 27 mwaka huu ilisema kwamba Rais Shein ameiagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuanza mchakato huo.
 
Meli inayotakiwa kununuliwa mbali ya kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1000 kwa wakati mmoja,pia iwe na uwezo wa kuchukua mizigo yenye uzito wa tani 100.
 
Katika mazungumzo yake na Bodi ya Shirika la meli Zanzibar Rais Dk. Shein aliwahakikishia wajumbe wa Bodi hiyo kuwa Serikali imedhamiria kununua meli ya uhakika ili kurahisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Zanzibar.
Mbali ya Bodi  ya Shirika la Meli, katika kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na  Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na  Mipango ya Maendeleo.
 Agizo la Rais Shein limeitaka Wizara yenye dhamana ya fedha kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanapata fedha kutoka vianzio vya ndani au nje ya nchi ama kutokana na  taasisi zinazohusiana na mambo ya fedha kununua meli hiyo.
Rais Dk. Shein ameagiza pia katika kipindi  kisichozidi miezi miwili ujumbe wa Serikali uende katika makampuni  yanayotengeneza meli nchini Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya utengenezaji wa meli hiyo.
 Wakitoa maelezo kwa Rais, Viongozi wa Shirika la Meli Zanzibar walisema kuwa meli mpya  yenye ukubwa inayotakiwa na Serikali huchukua muda wa mwaka mmoja kutengenezwa. 
Kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kuangalia mwelekeo na Mipango ya Shirika la Meli pia, kilijadili hali halisi ya meli za Shirika la Meli na  baadae kujadili  masuala ya ununuzi wa meli mpya itokayowaondoshea usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.

Kongamano la Tatu la Ushirikiano wa Kimaendeleo na Upunguzaji Umaskini Kati ya China na Afrika


 Waziri wa Nchi, Uhusiano na Uratibu, Mhe. Stephen Wassira (Kulia) akimsikiliza kwa makini Mhe. Fan Xiaojian, Waziri, Ofisi Kiongozi ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, inayohusika na masuala ya Maendeleo na Kupunguza Umaskini (Katikati). Kushoto ni Mkalimani wa Waziri huyo.Kongamano hilo la Tatu la Ushirikiano wa Kimaendeleo na Upunguzaji Umaskini Kati ya China na Afrika, linafanyika katika Hoteli ya White Sands.
 Naibu Katibu Mtendaji (Uzalishaji) wa Tume ya Mipango, Maduka Kessy (Katikati) akizungumza na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akizungumza na mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo Li Xin kutoka China.
 Wadau wa habari nao hawakuwa nyuma katika kunasa matukio ya Kongamano hilo.
 Gavana wa benki kuu Profesa Beno Ndulu kushoto akiwa katika konamano hilo la kupunguza umasikini pamoja na wadau wengine.
Washiriki wa Kongamano wakiwa makini kufuatilia mawasilisho na mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.Chanzo:fullshangweblog