Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


 

 Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein  amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,DKT .Abulhamid Yahya Mzee, DKT Shein amemteuwa 

1.Ali Salim Mchenga kuwa Afisa Tawala Mkoa wa Kusini,Unguja.

2.DKT Makame Ali Ussi kuwa Afisa Tawala Mkoa Kaskazini Unguja

3. Khamis Salim Mohd Shambi kuwa Afisa Tawala Mkoa Kaskazini Pemba.

 
Aidha DKT Shein amewateuwa 
1.Mohamed Abdulla Ahmed kuwa Afisa Tawala wa Wilaya Mjini,Unguja.
2.Omar Abdulla Juma kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kati,Unguja 
 3.Juma Abdulla Hamad kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kaskazini B,Unguja.
 
Katika Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo DKT Shein amewateuwa 

1.Abdi Khamis Faki kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar,
2.Hafidh Ussi Haji kuwa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar.
3.Seif Shaaban Seif kuwa Kamishna wa Mitaji ya Umma. 
4.Mwita Mgeni Mwita kuwa Kamishna wa Bajeti.

5.DKT Rahma Salim Mahfoudh kuwa Kamishna wa Ukuzaji Uchumi katika Tume ya Mipango ya Zanzibar 

 6.Bihindi Nassor Khatib kuwa Kamishna wa Fedha za Nje.

 
Wengine aliewateuwa katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano ni 

1.Capt Abdulla Juma Abdulla  kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Bandari 

 2.Abdi Omar Maalim ambae ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini.

 
Halkadhalika Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein Amewateuwa  wafuatao kutoka Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko  ambapo

1.Mwanahija Almas Ali kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC.
2 .Suleiman Juma Jongo Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC.
3 .Abdulmalik M .Bakari kuwa Ofisa Mdhamini wa ZSTC, Pemba 
 4.Khatibu Mwadini Makame kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la 5.Zanzibar(Zanzibar Bureau of Standards)

Advertisements

Launch of the Cecafa-Tusker Cup 2012 in Uganda


 

Cecafa General Secretary Nicholas Musonye receives a this year’s Cecafa-Tusker cup from EABL (U) Marketing Director Lemmy Mutahi at Serena Hotel Kampala on Tuesday. On the right is FUFA Vice President Livingstone Kyambadde.

Tusker Lager, one of the region’s major sports sponsors have this Tuesday announced a sponsorship package of USD 450,000 (About UGX 1.125.000.000) towards this year’s CECAFA –Tusker Cup to be hosted in Kampala.

The Council of East and Central Africa Football Association (CECAFA) has also fixed November 24 as the kick off date at Mandela National Stadium Namboole. The tournament will run through December 8. Cecafa General Secretary Nicholas Musonye who flew to Kampala on Monday attended the well organized event.

Unpacking the sponsorship during the Break Fast meeting at Serena Hotel in Kampala, Lemmy Mutahi the EABL (U) Marketing Director said the decision was taken with an ultimate aim of catapulting East African teams to the 2014 World Cup. He revealed that as sponsors they were happy to have the tournament hosted in Kampala. This year’s figure shows a 5% increase compared to last year’s release.

Musonye said the sponsorship package would cover the teams’ accommodation and air travels among others. A total of USD 60.000 will however go towards prize money with the winners taking USD 30.000, the runners up USD 20.000 and USD 10.000 for the third placed team. Musonye further revealed that the sponsors. All matches will be showed live on Super Sport.

The Sponsors (EABL) confirmed their long time engagement with Cecafa and praised the regional body for organizing excellent 2010/2011tournament in Tanzania.

Uganda (FUFA) have already formed a Local Organizing Committee to start preparations. The closing ceremony was attended by FUFA officials and the LOC and the top management of Uganda Breweries who have been mandated by EABL to sponsor the event in Uganda.

Later, Musonye had a long chat with the State Minister for Sports Hon. Charles Bakabulindi from his offices in Kampala. The minister pledged to support Cecafa and FUFA in organizing a successful event.

Kikao cha saba cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Mwaka 2012 chakutana Jijini Dar


Kikao cha saba cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Nchini kimekutana leo mjini Dar es salaamu kutathmini zoezi la kuhesabu Watu lililoanza usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita ya Tarehe 26/8/2012. 
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Saba cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini Dar es slaam.
Wajumbe wa Kikao hicho walikutana katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
 
Akitoa Taarifa katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Albina Chuwa alisema hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya Watu waliokataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu naMakazi pamoja na uandikishaji wa Vitambulisho wa Uraia. Dr. Alibina alisema Ofisi ya Takwimu ya Taifa ilizipatia Ofisi ya Polisi za Mikoa sheria na kanuni za Takwimu zinazoelezea kwa ufasaha haki za Mwananchi zinazompasa kujiandikisha kwenye zoezi la Sensa pamoja na zile zinazomkabili endapo atakataa kuhesabiwa. 
 
Alisema hatua hiyo ililenga kurahisisha utekelezaji wa sheria hiyo ndani ya kipindi cha zoezi zima la kuhesabu Watu katika kipindi hichi cha Sensa ya Watu na Makazi yam aka 2012. 
Kwa upande wao Mawaziri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Mapinduzi ya Zanzibar walisema jitihada zimechukuliwa katika kuipatia madodoso Mikoa ambayo ilikumbwa na upungufu wa Vifaa hivyo. 
 
Walisema hatua hiyo ya haraka imefanywa ili kuona zoezi la hesabu ya watu na makazi na uandikishaji wa Vitambulisho vya uraia linamalizika kwa kwa mafanikio kama lilivyopangwa. Walifahamisha kwamba jumla ya shilingi Bilioni 22.8 awamu ya kwanza tayari zimeshapelekwa Mikoani kwa ajili ya wasimamizi na Makarani wa sense na shilingi Bilioni 22.8 nyengine zitatolewa kabla ya Tarehe 30/8/2012. 
 
Aidha walizielezea baadhi ya changamoto zilizojichomoza ndani ya zoezi hilo ikiwemo baadhi ya watu katika shehia miongoni mwa hizo ni pamoja na Chwaka,kilindi, Nungwi,Pangawe, Fundo, Kilwa na Lindi. Halkadhalika Mawaziri hao waliwanasihi Wananchi kwamba kila mwana Jamii anahakikisha anafanikisha zoezi zima la sensa ya Watu na Makazi Hapa Nchini. 
 
 Naye Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alivipongeza Vyombo vya Habari Nchini kwa juhudi ilivyochukuwa ya Kuhamasisha pamoja na kutoa Elimu kwa Umma juu ya umuhimu wa Sensa a Watu. 
 
Balozi Seif alifahamisha kwamba ujumbe na Taaluma hiyo kwa kiasi kikubwa imewafikia Wananchi kwa asilimia kubwa kama ilivyotarajiwa. “ Waliokataa kuhesabiwa kwenye zoezi hilo la kuhesabu watu kwa kweli wana lao”. Alielezea Mwenyekiti huyo Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Nchini.

Taswira Mbali Mbali Za Mkutano Wa Chadema Reading


 

 

                                 Katibu Wa Chadema Uk Libe Musiba akiwa na Mwenyekiti

                       SALIM akikabidhiwa kadi yake

                                                       Kamanda Lukosi

Kamanda Lema alihutubia mkutano kwa njia ya simu

         Mwenyekiti wa wanawake Kamanda Jessica Maduhu

                Picha na Kamanda Lukosi- M4C UK.

Clouds Media Group yatoa msaada kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani Center


 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akikabidhi sehemu ya msaada kwa muwakilishi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira cha Amani Center kilichopo nje ya mji wa Moshi,kwa mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum,Msaada huo umetolewa jioni ya leo na kampuni ya Clouds Media Group,ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuisaidia jamii.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Amani Center wakishuhudia tukio hilo,ambalo pia limewahusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya,akiwamo Juma Nature,Joe Makini,Bob Junior,Shetta,Ferouzi,Lina na wengineo ambao pia watatumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha la Serengeti   Fiesta 2012,kwenye uwanja wa chuo cha Ushirika.
 Pichani anaezungumza nia Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akizungumza kwa ufupi ikiwemo sambamba na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group iliombatana na baadhi ya wasanii,kwa namna ambavyo wamekuwa wakiijali jamii kwa namna moja ama nyingine,shoto ni Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga na mwisho shoto ni mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum pamoja na Afisa Ustawi wa jamii wa Moshi,Bwa. Sammy Mulemba.
Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga akimkaribisha Mkuu wa Wilaya na wageni wengine waalikwa mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,kwenye moja ya darasa la kituo hicho cha Amani Center.
Ofisa Mawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akitoa maelezo na historia fupi ya kituo hicho kwa baadhi ya wasanii walioshirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho jioni ya leo.
Ofisa Mawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Moshi mjini,Mh.Dr Msengi alipowasili kwenye kituo hicho kwa niaba ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula.
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kushirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada huo.Chanzo:lukazablog

Hatimaye Kalala arejea Twanga Pepeta na zawadi nono


 
Kalala Junior akizungumza na katika mkutano wa utambulisho kwenye ukumbi wa MangoGarden, kulia ni kiongoz msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza huku kushoto ni Msemaji wa ASET, Mohamed Pizaro na meneja wa ASET, Hassan Rehani.
Kalala Junior ( Katikati) akiweka hadharani vionjo vya wimbo wake mpya, Nyumbani ni Nyumbani kwenye mkutano na waandishi wa habari  akiwa na wanenguaji wa bendi hiyo, Frida Joseph aka Beckham, Sabrina Mathew na Mary Hamis aka Mary Kimwana wakionyesha staili yao mpya.
Na Mwandishi wetu
UONGOZI wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Mapacha Watatu.
Mwimbaji huyo maarufu alisema kwa  fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao  kwa sasa upo katika hatua ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka  kuamua kurejea Twanga,”  alisema Kalala.
Alisema kuwa  ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka  fadhira za ASET ambapo ndipo alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba  wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki wengi wa muziki wa dansi.
Afisa Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani ni Nyumbani .
Pizaro alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa wanatumikia bendi nyingine.
Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
“Karibu nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza.