Na Gazeti la mwananchi:Walimu wazidi kuitilia ngumu Serikali

 
MUKOBA ASEMA WATAGOMA HATA BAADA YA LIKIZO, ASKOFU RUWA’ICHI ASEMA TUNAKOELEKEA SIKO
 
Rais wa CWT, Gratian Mukoba
Waandishi wetu, Dar, mikoani
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa tamko kikisema hata kama shule zitafungwa wiki hii, mgomo utaendelea baada ya kufunguliwa endapo Serikali itakuwa haijatimiza madai yao.

Tayari mgomo huo umesababisha athari kubwa katika mfumo wa utoaji elimu nchini kuanzia msingi na sekondari na jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema Dar es Salaam kwamba mgomo huo hautaathiriwa na kufungwa kwa shule.

 
“Mgomo huu hauna ukomo, ni Serikali tu ndiyo itakayoamua uishe au uendelee. Tukipewa nyongeza tunazotaka utaisha lakini tusipopewa utaendelea milele,” alisema Mukoba. Jana ilikuwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa mgomo huo.
 
Alisema mgomo huo ni wa mafanikio makubwa, kwa sababu unahusisha asilimia 95 ya walimu… “Walimu wachache wanaoendelea kwenda shuleni ni waoga, wanafiki wenye kujipendekeza ili wapate vyeo na wanasaliti wenzao wanaodai haki zao,” alisema.
 
Rais huyo wa walimu alidai kuwa walimu hao wanaoendelea na kazi ndiyo wanaosababisha vurugu kwenye baadhi ya shule kwa sababu wao wamewaagiza walimu kubaki majumbani.
 
“Tunawaagiza walimu waendelee kubaki majumbani kwani wanaweza kusingiziwa na mwajiri kwamba wanawachochea wanafunzi kuandamana na kuharibu vifaa vya shule,” alisema.
Mukoba alisema mgomo huo ni halali na iwapo walimu waliogoma wataadhibiwa, chama kitafuata taratibu za kisheria kuwatetea wanachama wake.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s