Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye Awaasa Waislam Waadilifu Kuiombea Nchini Ya Tanzania idumu na Amani

 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiongea na Wajumbe wa Nyumba Kumi Mkoani Morogoro
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaasa Waislam kuutumia uadilifu wao kuiombea Tanzania iendelee kuwa nchi ya  amani na utulivu.
 
Kimesema amani ikishamiri hapa nchini, Waislam kama Watanzania wengine wataunufaika nayo kwa kuweza kufanya  mipango yao ya kuabudu Mungu na ya maisha yao ya kila siku bila mashaka tofauti na amani ikitetereka.
 
Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye wakati akizungumza na  mabalozi wa nyumba kumi mkoani Morogoro, baada ya kuwafuturisha jana, futari aliyoandaa kwenye ukumbi wa shule  ya  Sekondari Forest mjini hapa.
 
“Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, tumeona kwamba faradhi hii ya Funga ya Mwezi wa Ramadhani mnayotekeleza,  pamoja na kuwa ni muhimu sana kwenu kama Waislam lakini pia ni muhimu sana kwa taifa letu kwa sababu tunaamini  uchamungu huzaa uadilifu na uadilifu ni chanzo pia cha kudumisha amani na utulivu tulio nao hapa nchini, hivyo kwa  niaba ya Chama nikaona ni vizuri tukafuru pamoja jioni ya leo”, alisema Nape.
 
“Nachowaasa Waislam mliojumuka hapa na wale ambao hatukubahatika kuwa nao kwenye futari hii, endeleeni  kuutumia uadilifu wetu mliouithibitisha mbele za Mungu kwa funga hii, kuiombea nchi yetu iendelee kuwa na amani na  utulivu, maana amani ikitoweka huathiri kila kitu ikiwemo ibada”, alisema Nape.
 
Nape aliwaomba waislam katika dua zao pia kuwaombea pepo wabaya wawatoke, watu ambao alisema wamekuwa kila  kukicha wanatamani amani iliyopo nchini itoweke kutokana na uchu wa madaraka.
 
Mapema akimkaribisha kuzungumza kwenye futru, Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda  alikishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa uamuzi wake wa kuamua kuwafurutisha wajumbe wa nyumba kumi wa mkoa wa  Morogoro akieleza kwamba tukio hilo limeongeza mshikamano kwa wana-CCM na wananchi kwa jumla mkoani humo.
 
Alisema, zaidi ya wajumbe 450 kutoka wilaya za mkoa huo, walifanikiwa kuhudhuria kwenye futari hiyo, na kukitaka  Chama kujijengea uitaratibu huo hata kwa mikoa mingine.
 
“Uzuri wa futru hii ni kwamba  mbali na kwamba ni ibada kwa waislam, lakini pia inatuweka pamoja waislam na  wasiokuwa waislam kwa kuwa watu wamealikwa hapa bila kutazama dini zao au kuchagua waliofunga na ambao  hawakufunga kama Mzee wangu pale mkuu wa mkoa wa zamani wa mkoa huu (Morogoro) Steven Mshishanga”,  alisema, Sixtus.
 
Mbali na Mashishanga futari hiyo ilihudhuriwa pia na  Mkuu wa mkoa wa Morogoro,  Joel Bendera, Mwanasiasa wa siku  nyingi mkoani Morogoro ambaye pia amewahi kuwa Mbunge, Semindu Pawa na viongozi mbali mbali wa CCM mkoani 
humo.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s