Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari, Ibada Ya Kumuaga Na Kusafirisha Mwili Wa Fred Mtoi…!


Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari, Ibada Ya Kumuaga Na Kusafirisha Mwili Wa Fred Mtoi…!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI IBADA YA KUMUAGA NA KUMSAFIRISHA MTANGAZAJI WA BBC FRED MTOI
Idhaa ya Kiswahili ya BBC London inawaarifu wapenzi wa BBC, ndugu, jamaa na marafiki hasa walioko Uingereza kuwa, ibada ya kumuaga mtangazaji wake Fred Mtoi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba 2012 itakuwa Jumamosi tarehe Mosi Disemba 2012.
Ibada hiyo itafanyika katika Kanisa la St. Anne’s Lutheran mjini London kuanzia saa tano kamili asubuhi.
Anwani ya Kanisa ni: St Anne’s Lutheran Church, Gresham Street, London, EC2V

Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege ya Shirika la British Airways.

Mwili unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumanne saa moja asubuhi.
Mipango ya Ibada na mazishi nchini Tanzania inafanyika nyumbani kwa wazazi wake Tabata Maduka Manne jijini Dar es salaam. Ibada ya kumuaga Fred itafanyika katika kanisa la Lutheran Tabata Kuu saa saba mchana siku ya Jumatano tarehe 5 Disemba 2012. Maziko yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam saa tisa alasiri.

Fred alianza kazi ya utangazaji Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa masomo. Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya Uzamili kuhusu ‘Digital Media’ katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki pia katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na aliyepatana na wote. Alikuwa mtangazaji mtulivu na akishikilia kazi alihakikisha anaimaliza vema.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Fred atakumbukwa kwa umahiri wake katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred hadi Tanzania.
Pia shukran kwa wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha mipango ya yote kuhusu msiba huu.

Imetolewa na:
Zawadi Machibya
Mratibu wa Mazishi
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
London
Kwa maelezo zaidi piga simu
+44 795 260 7038

Tanzania keen on Kenyan polls


The Deputy Leader of the Opposition in the National Assembly, Mr Zitto Kabwe Tanzania keen on Kenyan polls
By Jelimo Chelagat

Tanzania is keenly watching Kenya as she inches toward the March 4 general election, says Zitto Kabwe, Tanzania’s Deputy leader of opposition.

The Deputy Leader of the Opposition in the National Assembly, Mr Zitto Kabwe

Mr Kabwe expressed that Tanzania is disappointed with the turn that political pacts are taking.

“We are disappointed that alliances are being formed on tribal lines,” said Kabwe.

He added that in Tanzania such moves would be a death card for any politician since the country shuns tribalism.

Speaking on Thursday at Standard Group’s offices on Mombasa Road when he paid a courtesy call, Kabwe stated that Kenya is a key trade partner of Tanzania and thus the events in Kenya are of importance to his country.

Kabwe, who is the MP for Kigoma North, expressed concern that tribal tendencies could find their way to the neighbouring country.

Citing the secessionist calls by Mombasa Republican Council which have been echoed by groups in Zanzibar as example, he said that occurrences in Kenya could spread to other areas in the East African region.

Addressing leaders, he encouraged them to embrace issue-based politics and shun the dangerously divisive politics of tribe.

“We are watching Kenya closely… We wouldn’t like to see what happened in Kenya on 20007 again,” said Kabwe.

Though reluctant to speak on the ICC cases facing Presidential aspirants Uhuru Kenyatta and William Ruto, Kabwe expressed that the same could not take place in Tanzania.
Read more »

Nov 30 Polisi wajeruhi kwa mabomu Jijini Dar es Salaam, Rufiji


POLISI wamewajeruhi watu watatu kwa mabomu, mmoja kati yao akiwa katika hali mbaya katika

wamewajeruhi watu watatu kwa mabomu, mmoja kati yao akiwa katika hali mbaya katika matukio mawili tofauti ya kusambaratisha mikusanyiko iliyotokea Tegeta, Dar es Salaam na Rufiji mkoani Pwani.

Aliyejeruhiwa vibaya ametambuliwa kuwa mkazi wa Tegeta, John Paul ambaye baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala na baadaye Muhimbili.

Tukio la Tegeta lilitokea wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wananchi waliokuwa wakipinga operesheni ya kuwaondoa katika hifadhi ya barabara katika eneo hilo saa nne asubuhi baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya Mwankinga wakiwa na polisi waliyolikamata gari la mkazi mmoja wa eneo hilo.
Hali hiyo ilizua ubishi na baadaye vurugu baada ya wakazi hao kutaka gari hilo lisichukuliwe na polisi.Kwa habari zaidi bofya na Endelea,….>>>>>

Jaji Chande Aikwepa Kesi Ya Lema


JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amejitoa kusikiliza rufaa ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, badala yake nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.
Kujitoa kwa jaji mkuu kumekuja ikiwa zimebaki siku tano kusikilizwa upya kwa rufaa hiyo Desemba 4, mwaka huu, baada ya awali Mahakama ya Rufani, kuona rufaa hiyo ilikuwa na dosari.
Mahakama hiyo ilikubali hoja ya wajiburufaa kuwa rufaa hiyo ilikuwa na dosari kutokana na tofauti ya vifungu vya sheria vilivyotumika katika hukumu iliyomvua ubunge Lema na vilivyotumika katika hati ya kukaza hukumu, iliyowasilishwa mahakamani sambamba na rufaa hiyo.
Hata hivyo, kilichomwokoa Lema ni kifungu cha 111 cha Kanuni za Mahakama, ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa chini ya kanuni hiyo, dosari hizo zinaweza kurekebishwa.
Jaji Chande ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo la majaji watatu katika kesi hiyo akiwamo Salum Massati na Natalia Kimaro.
Jaji Mkuu aliingia kwenye kesi hiyo akichukua nafasi ya Jaji Mbarouk Salim Mbarouk aliyekuwa amepangwa awali, ambaye sababu za kuondolewa hazikuwekwa wazi.
Wakili wa Lema, Method Kimomogoro alithibitisha kuwa amepata taarifa kuwa jaji mkuu hatasikiliza rufaa hiyo na badala yake Jaji Luanda ndiye atachukua nafasi yake.
“Ni kweli jaji mkuu hatakuwapo kusikiliza rufaa ya Lema nimewasiliana na Msajili Dar es Salaam ameniambia hatokuwepo kwenye hilo jopo,” alisema Kimomogoro na kuongeza:
Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alisema “Huu ni utaratibu wa kawaida wa mahakama kwa kuwa huenda jaji mkuu akawa amesafiri au ana shughuli nyingine.”
Wakili wa wajiburufaa, Alute Mughwai alisema hajapata taarifa kama Jaji Mkuu ameondolewa kwenye jopo hilo kwa kuwa huo si utaratibu wa mahakama kutoa taarifa hizo.
“Mahakama huwa haitoi taarifa, zinawekwa (taarifa) kwenye ubao wa mahakama siku ambayo rufaa inasikilizwa,” alisema.
Aliendelea, “Jaji yeyote atakayepangwa sisi hatuna tatizo kwa kuwa wote ni majaji, wewe uko huko Dar na mimi niko huku bara (Arusha), hivyo unaweza ukazipata taarifa zaidi huko kwa kuwa ndiyo uko jikoni Dar.”

Palestinians seek historic state backing at U.N.


 
Palestinian President Mahmoud Abbas (L) shakes hands with United Nations Secretary General Ban Ki-moon at the U.N. headquarters in New York November 28, 2012. (Reuters)
Palestinian President Mahmoud Abbas (L) shakes hands with United Nations Secretary General Ban Ki-moon at the U.N. headquarters in New York November 28, 2012. (Reuters)
 
By AL ARABIYA WITH AGENCIES
 
Palestinian leader Mahmud Abbas will head to the U.N. General Assembly on Thursday with huge backing for his bid for upgraded diplomatic status despite strong U.S. and Israeli opposition.
 
Abbas will ask for the Palestinians to be recognized as a U.N. “non-member observer state” and indicate his conditions for talks with Israel in a key speech to the 193-member assembly, set to convene at 3:00 pm (2000 GMT).
 
The Palestinians say 132 countries recognize their state bilaterally, but some of those are expected to abstain while many European nations are expected to vote in favor even though they have not recognized a Palestinian state.
 
Thursday’s motion requires a simple majority of those members present and voting in order to pass, and the bid is widely expected to be approved.
 
The Palestinian leadership is determined to make the 65th anniversary of a U.N. resolution on the division of Palestinian territory a “historic” landmark in their quest for an independent state.
 
The United States, a staunch ally of Israel, has launched an aggressive campaign against the bid, warning that the vote will do nothing to improve the prospects for new peace talks aimed at ending the decades-long conflict.
 

MASELE CHA POMBE NAE ‘AMKACHA’ SHARO MILIONEA …ZE COMEDY, ORIJINO KOMEDI NAO HAWAJAONEKANA MAZISHINI


 

MCHEKESHAJI Chrispin Masele “Masele cha pombe”, jana alikuwa ni miongoni mwa sura chache zilizokosekana kwenye mazishi ya Sharo Milionea.

 

Masele ambaye ni msanii wa Al Riyami Production (mabosi wa zamani wa Sharo), ni mmoja kati ya wasanii waliofanya kazi nyingi na kwa ukaribu sana na Sharo Milionea.

Wasanii wa Al Riyami waliiambia Saluti5 kuwa Masele yuko safarini Dodoma pamoja na Mkurugenzi wao Khalfan Abdallah.

Wasanii wengine wa vichekesho walioshindwa kuhudhuria mazishi ya Sharo, hususan wale ambao vituo vyao vya kazi ni Dar se Salaam ni pamoja na Ze Comedy (EATV) na Orijino Komedi (TBC1).

Ukiondoa wasanii hao, karibu wasanii wote wa sanaa za maigizo sambamba na wale Bongo Fleva, walihudhuria mazishi ya kihistoia ya Sharo Milionea.Chanzo:www.saluti5.com

University of Dar es Salaam ranked 6th best University in Africa


According to a new ranking released by Africa.com, University of Dar es salaam is the 6th best University in Africa. Cairo University is the still the best University in Africa.

See the top 10 best Universities in Africa below…
1. Cairo University – Egypt
2. American University in Cairo – Egypt
3. Mansoura University – Egypt
4. Makerere University – Uganda
5. University of Nairobi – Kenya
6. University of Dar es Salaam – Tanzania
7. University of Botswana – Botswana
8. University of Ghana – Ghana
9. University of Lagos – Nigeria
10. Ashesi University – Ghana