NBC yazindua kampeni ya “Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI”

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru
(kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Lemweli Shiwakwe
katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi
wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo
viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (wa
pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo, katika
Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa
kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo
viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.
Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa NBC, Jane Dogani.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kushoto) akisaidia
kuhesabu pesa ili kumhudumia mmoja wa wateja wa NBC wakati wa uzinduzi
huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (katikati) akiwa
pamoja na baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa
kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo
viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.
…………………………………………………………………..
NBC jana ilizindua kampeni ya kuboresha huduma kwa wateja ambayo itaendelea hadi mwisho wa mwezi Novemba 2012 na kuhusisha uongozi mzima wa NBC. Kampeni hiyo ijulikanayo kama kama Leadership in action – I CARE, au kwa Kiswahili “Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI”, inalenga katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja NBC. Ni siku ambayao lengo lake kuu ni kwa Uongozi wa NBC kutoa huduma kwa wateja.
Kampeni ilizinduliwa katika tawi la NBC Corporate, lililopo jijini Dar es Salaam. Ili kuzindua rasmi kampeni hii Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Lawrence Mafuru alikuwa Kiongozi wa kwanza wa benki kwenda tawini kuongea na wateja na kutoa huduma. Bw Mafuru alizungumza na wateja wa NBC juu ya masuala mbali mbali ikiwamo pia kuridhika kwao na huduma ya NBC na kama wana mapendekezo yoyote.
“Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI” itafanyika kwenye matawi kadhaa ya NBC. Kampeni hii itakayofanyika kati ya Novemba 19 na 30 2012 itashirikisha jumla ya matawi 25 nchini. Matawi 18 yakiwa jijini Dar es salaam na matawi 7 mengine yakiwa mkoani.
Kampeni hii ni sehemu ya Kampeni nyingine ya kibenki inayolenga kurahisisha maisha ya wateja wake kwa kuwapatia huduma bora zaidi. “Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI” inakusudia kuweka wateja wa NBC mbele na kuhakikisha wanaridhika na huduma zitolewazo na benki hiyo na hatimaye kuwa karibu zaidi na wateja wake.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s