SELF SHABAN AKA MATONYA BUSSINESS ANAKUJA NA ZILIPENDWA…!

 


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Seif Shaban ‘Matonya Bussiness ‘, ni mmoja wa wasanii wachache wenye mafanikio ambayo kwa njia moja au nyingine ni mfano wa kuigwa kwa wengine walioko kwenye tasnia hiyo.

matonya ambaye nimekutana naye juzi kwenye mtaa wa Zaramo  katikati ya jiji la Dar es salaam ,anasema kupitia muziki, amefanikiwa kupata mafanikio mengi ikiwemo kutembea na kufanya muziki katika nchi mbalimbali za Ulaya, Afrika na kusaidia kumtangaza vema.

Nyota huyo alianza kujiingiza katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya 2000, na baada ya miaka 10 amefanikiwa kuwa na mafanikio makubwa kwenye anga hizo.

Msanii huyo alianza kutambulika vema kwenye tasnia hiyo baada ya kuachia wimbo wa Vailet, ambao ulimuweka pazuri katika tasnia hiyo, ambayo sasa ana mafanikio ambayo ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wenzake hususani wanaoinukia.

Baada ya kutoka na kibao hicho, pia alichia vibao lukuki kikiwemo kinachofanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na luninga cha Ajali Kazini pamoja na Mapenzi Kamari.Kwa sasa msanii huyo anatamba na traki yake mpya inayoitwa “Zilipendwa”.

“Zilipendwa  ni taki yangu mpya , ipo redioni na kwenye vituo vya runinga , nashukuru mwenyezi Mungu inafanya vema, nimeirekodi kwenye stuidio ya Burn  Records  chini ya mtayarishaji anayeitwa Sheddy  Clever ambapo video wamefanya kampuni ya Apex chini ya usimamizi wa Pablo .” Alisema Tonya B.Pia unaweza kuzama….http://wwwmasterkif.blogspot.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s