Kenya kuchunguza ghasia za askari huko Garissa

 
Serikali ya Kenya inachunguza ghasia za vurugu ambazo ilifanywa na askari wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya huko Garissa kufuatia kuuliwa kwa wenzao watatu siku ya Jumatatu, Waziri wa Ulinzi Mohamed Yusuf Haji alitangaza siku ya Jumanne (tarehe 20 November).
 
Moshi watanda mandhari wakati wakaazi wa Garissa wakitembea juu ya takataka za soko lililoharibiwa wakati wa mapambano na wanajeshi kutoka Vikosi vya Ulinzi vya Kenya. [Na Bosire Boniface/Sabahi]
 
Haji alisema kuwa hakuamrisha operesheni ya usalama iliyopelekea uharibifu wa mali na kuchomwa moto kwa soko kuu la Garissa. “Nimeamrisha uchunguzi ufanyike ambao utapelekea hatua za kinidhamu dhidi ya wakosaji wa matendo haya ya kikatili,” Haji aliwaambia waandishi wa habari.
 
Pia aliiomba jamii kuvisaidia vikosi vya ulinzi ili kuwatambua wanamgambo wa al-Shabaab waliohusika na mashambulizi ya karibuni ya kigaidi katika wilaya yao.
 
Watu wenye silaha wasiojulikana waliwaua wanajeshi hao wakati walipokuwa wakibadilisha mpira uliotoka upepo karibu na shule ya msingi ya Garissa, kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Kenya Cyrus Oguna. Mauaji hayo ya risasi yalikuja siku tatu baada ya watu wenye silaha wasiojulikana walipowaua polisi
 
wawili wa uchunguzi waliokuwa wakitembea katika soko la Mugdi la Garissa.
 
Wakaazi wakikagua hasara kwa biashara zao ndogondogo katika ofisi ya kuuzia tiketi za basi ya Gateway huko Garissa. [Na Bosire Boniface/Sabahi]
 
Kiongozi mkuu wa al-Shabaab Abduaziz Abu Musab alisema kuwa “inawezekana baadhi ya wanaopendelea dhamira yetu walifanya hivyo peke yao” katika mauaji ya askari wa Garissa, kwa mujibu wa AFP.
 
Baada ya mauaji hayo, wanajeshi kutoka kambi ya kijeshi ya Garissa walimiminika mjini, wakawapiga na kuwakamata wakaazi, mashuhuda waliiambia Sabahi. Ghasia za wanajeshi hao pia zilisababisha upingaji wa vurugu na vita vya mitaani na maafisa wa usalama karibia siku nzima Jumanne.
 
Mmoja auawa, makumi wajeruhiwa
 
Mkazi wa Garissa Mustafa Khalib Mohammed, mwenye umri wa miaka 28, aliiambia Sabahi kuwa askari walifyatua silaha zao hewani siku ya Jumatatu na baadaye kuwapiga wananchi. “Waliwalazimisha watu wote kufunga biashara zao na ofisi,” alisema. “Walidiriki hata kuingia majumbani na mahotelini, wakiwatimua wakazi na kuwalazimisha kuogelea katika madimbwi yaliyosababishwa na mvua kubwa ilionyesha usiku uliotangulia.”
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s