Vietnam na Zanzibar zakubaliana kuimarisha uhusiano

 

 
Hanoi,Vietnam 23.11.2012
 
ZANZIBAR na Vietnam zimekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kukuza sekta za maendeleo na uchumi huku Vietnam ikiahidi kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha inafikia malengo yake iliyojiwekea katika kuimarisha sekta za maendeleo na uchumi .
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, wakaribishwa katika Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja. [Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein alisema kuwa ipo haja ya kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzaniaikiwemo Zanzibar na Vietnam hasa katika sekta za maendeleo na uchumi.
 
Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais wa Vietman Mhe. Bi Nguyen Thi Doan huko katika ukumbi wa Ikulu ya nchi hiyo mjini Hanoi.
 
Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Vietnam kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika uimarishaji wake wa uchumi na pamoja na sekta za maendeleo.
Dk. Shein alisema kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo kati ya Zazibar na Vietnam ni pamoja na sekta ya uvuvi, kilimo, utalii, uimarishaji wananchi kiuchumi, biashara pamoja na sekta nyenginezo.
 
Aidha, Dk. Shein amueleza Makamu huyo wa Rais kuwa Tanzania na Vietnam zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu tokea miaka ya 1960 na zimeweza kuungana mkono katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo, kiuchumi na hata kisiasa.
 
Dk. Shein alimueleza kingozi huyo hatua zinazochukuliiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo na uchumi na mafanikio yaliofikiwa katika kutekeleza Dira ya 2020 pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi a Kupunguza Umasikini (MKUZA).
 

Kwa upande wa kilimo Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Tanzania imeweka mikakati maalum ya kuimarisha sekta ya kilimo ambapo kwa upande wa Zanzibar Serikali mechukua juhudi kubwa katika kuhakikisha sekta hiyo inapewa kipaumbele.

 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s