TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Mnamo mwezi Octoba, 2012 Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi wema ikihusu uwepo wa mtandao wa watu wanaojipatia fedha kutoka kwa wananchi, ili waweze kuwapatia ajira katika Jeshi la Polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za ajira ndani ya Jeshi la Polisi.

Kwa kuwa mfumo wa ajira katika Jeshi la Polisi ni wa wazi na unafuata utaratibu ulioainishwa katika kanuni za kudumu za Jeshi la Polisi (Police General Orders) na Sera ya ajira ya utumishi wa umma, taarifa hizo zilisaidia upelelezi wa kina kuanza kufanyika na kufanikiwa kumtia mbaroni bwana mmoja anayefahamika kwa jina maarufu Komba na tayari mtu huyo amefikishwa mahakamani.

Kwa vile Jeshi la Polisi linaamini kwamba, mtuhumiwa Komba na wenzake wasingeweza kufanikisha mpango wao bila ushiriki wa watu wengine wa ndani na nje ya Jeshi la Polisi, kwa sababu hiyo, taratibu za ndani kulingana na Police General Order (PGO) tayari zimeanza ili kuchunguza na kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kuhusika na mtandao wa utapeli wa bwana Komba.

Kwa taarifa hii tunawakumbusha wananchi wote kwamba mfumo wa ajira ndani Jeshi la Polisi ni wa wazi na unafuata taratibu na kanunizake. Wananchi wanahimizwa kufuata taratibu na maelekezo yanayotolewa katika tangazo la ajira linapotolewa kupitia vyombo vya habari yakiwemo magazeti, radio, luninga ama mtandao wa Polisi www.policeforce.go.tz.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wote wenye malalamiko au taarifa kuwa walitoa fedha ili kupatiwa ajira na matapeli hao au mawakala wao, kutoa ushirikiano utakaowezesha  Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi na hatimaye ushahidi uweze kupatikana kusaidia katika kuthibitisha kesi iliyopo mahakamani au kwa kuwapata wengine wote watakaothibitika kulingana na taarifa zitakazopatikana.

Tunaomba taarifa zitumwe kwa ujumbe mfupi (sms) au kupiga simu ya IGP kupitia namba 0754 785557 ama kuwasilisha taarifa hizo moja kwa moja Makao Makuu ya Polisi ghorofa namba 4 ofisi ya malalamiko.

 Imetolewa na

Advera Senso (ASP)- Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s