Na Gazeti la Mwananchi:Kumekucha mabilioni ya Uswisi

Na Gazeti la Mwananchi:Kumekucha mabilioni ya Uswisi

SERIKALI imeamua kuunda kikosikazi kitakachohusisha Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa (Interpol) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kuanza uchunguzi kuhusu Watanzania wanaotuhumiwa kuficha kiasi cha Sh314 bilioni nchini Uswisi.

Mwanasheria mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema.

Hatua hiyo ya uchunguzi inatokana na Bunge kutoa maazimio ya kuitaka Serikali kufuatilia sakata hilo katika kikao chake kilichopita mjini Dodoma na kutoa majibu katika kikao cha Bunge cha Aprili mwakani.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.”

Jaji Werema alisema kuwa Serikali imeshapiga hatua katika kufanya uchunguzi huo.

“Tumepiga hatua katika suala hili, ila ukianza kusema sana utakuwa unaharibu. Tumeamua kuwa na kikosi maalumu cha upelelezi kitakachoshirikisha Idara ya Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Wizara ya Fedha na wachunguzi binafsi wakiwamo Polisi wa Kimataifa (Interpol) pamoja na Benki ya Dunia (WB).

“Serikali inaweza kuwashirikisha watu wengine kama Benki ya Dunia (WB) na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kusaidia uchunguzi huo.”

Aliongeza kuwa katika timu hiyo, wameamua kumshirikisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutaka ukweli wa sakata hilo.

“Tumeamua kulifuatilia jambo hili, kama tutafanikiwa litakuwa jambo jema. Kama hatutafanikiwa tutakuwa tumejaribu,” alisema.

Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi.
Read more »

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s