Walimu Wakimbia Shule Kwa Kubakwa Na Wanafunzi

 
 

 WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.

 
Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
 
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.
 
Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.
 
“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.
 
Mwalimu huyo alidai kuwa walimu: http://www.mwananchi.co.tz/
Advertisements

2 Comments

  1. Waalimu poleni sana na hayo ila Mungu yupo na serikali kama haiwasaiidii acheni kazi katafuteni kwingine na kama mna wajua hao vijana walio wabaaka nendeni mka washitaki kwa pamoja mahakamani sheria ichukue mkondo wake , salam aleikum

    Like

    Reply

  2. Hao waalimu ni vilaza kwa nini wasimshike mmoja wa wanafunzi hao wakampa kichapo mpaka akazimia?hilo lingekua funzo kwa wote hata mzazi naye akija apewe kichapo bila kuogopwa aieeeeeee!!!!!

    Like

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s