Mbunge Sugu awasifu wanaohama CCM kwenda Chadema

 

 
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu “Sugu” amesema kuwa kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi mkoani Mbeya, kuendelea kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM),na kukimbilia Chadema ni ishara kwamba majimbo yote 11 ya mkoani hapo yanakwenda kutawaliwa na Chadema mwaka 2015.
 
Sugu alisema kuwa wananchi wameendelea kujitambua kuwa kwa kipindi kirefu walikuwa wanapotea njia huku wakiendelea kudhulumiwa na CCM hivyo kuchukua uamuzi mgumu wa kukihama kwa kasi chama hicho.
 
Alisema hiyo ni dalili tosha kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hawatafanya makosa tena ya kuendelea kuwachagua wabungeakupitia CCM na badala yake watakiunga mkono Chadema kwa kushika majimbo yote ya mkoani hapa.
 
Sugu alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Saza wilayani Chunya kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa mahususi kwa kampeni za chama hicho kwa mgombea wa kiti cha Mwenyikti wa kijiji hicho zinazotarajiwa kufanyika Desemba 9 mwaka huu.
 
Alisema kuwa CCM ilionekana kutawala kwa kipindi kirefu huku wananchi wakilazimika kufanya hivyo kwa kuwachagua viongozi wao kutokana na kutokuwapo kwa chama makini chenye uwezo wa kuwatetea wananchi wake ndiyo maana hadi leo hii wananchi wanazidi kuwa maskini wa kutupwa.
 
“Nataka kusema hivi ndugu zangu wa Saza, kuwa kutokana na mwamko wenu wa kijitambua kuwa CCM ndio adui namba moja wa kufilisi mali zenu, hivyo kuchukua uamuzi mgumu wa kukihama na kuja Chadema ni ishara kwamba hamtafanya makosa tena 2015,’’ alisema.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s