Sita kutoka Heroes waitwa Taifa Stars

WACHEZAJI sita wa Zanzibar Heroes, wakiongozwa na Nadir Haroub wameitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.
 
Wachecahi wa Zanzibar Hero’s 
 
Stars na Chipolopolo zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 22. Chipolopolo inajiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwakani nchini Afrika Kusini.
 
Tangu Kocha Kim Poulsen aichukue Stars kutoka kwa mtangulizi wake, Jan Poulsen Mei mwaka huu, hakuwahi kuwaita wachezaji hao na amefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na kiwango chao kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika hivi karibuni Kampala, Uganda.
 
Nyota hao wanaoichezea timu ya Taifa ya Zanzibar, waliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo wakiifunga Stars kwa penalti katika mchezo wa kuwania nafasi hiyo.
 
Wachezaji sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kampala, Uganda, Kipa Mwadini Ally (Azam), Nassoro Masoud Cholo ( Simba), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ( Yanga), Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis wote wa Azam.
 
Poulsen alisema kuitwa kwa wachezaji hao kunafuatia kiwango cha kuridhisha kwenye mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni.
 
Nadir Haroub kwa kipindi sasa alikuwa ameachwa na Kocha Paulsen baada ya kushuka kiwango hivyo pongezi pekee zimwendee Cannavaro kwa kufanya bidii na kutovunjika moyo wakati alipoachwa na kumwonesha Kocha kivitendo kitu gani anakikosa ikiwa hayumo katika timu ya taifa na si maneno.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s