HADITHI YA TYSON KUWA DEMU SAWA NA SIKUKUU YA WAJINGA, HAINA UKWELI WOWOTE

 

 

 
 

Mitandao kadhaa barani Afrika imechapisha habari za kutengenezwa kuhusu bingwa wa zamani wa ndozi za uzito wa juu, Mike Tyson kuwa amebadilisha jinsia yake. (Kutoka mwanaume na kuwa mwanamke).
Makala ya kwanza ilionekana kwenye tovuti ya vituko ya Uingereza, NewsBiscuit, mwishoni mwa Novemba.
 
Baada ya hapo habari hizo zikaibukia Zimbabwe kupitia gazeti la Standard Jumapili kabla ya kufuatiwa na tovuti ya SpyGhana ya nchini Ghana Jumanne hii.
NewsBiscuit imetamba kuwa tovuti yao ilitembelewa na wasomaji wengi kutoka Afrika kufutaia habari hizo kuandikwa sana na mitandao ya Afrika.
“Tulikuwa na zaidi ya nusu ya wageni  kutoka Afrika katika siku chache zilizopita na tulitarajia hivyo kwa mwezi mzima,”  mwandishi wa vituko, John O’Farrell kutoka NewsBiscuit aliiambia BBC.
Alisema hadithi imetazamwa kwa  zaidi ya mara 50,000 katika siku chache zilizopita, ikiwa ni mara 20 zaidi ya mara ni kawaida.
Makala hiyo ilisema kuwa bondia huyo sasa atajulikana kama Michelle na kwamba alijisikia vizuri baada ya kufanyiwa operesheni iliyochukua masaa 16.
Tafiti zinaonyesha kwamba nchini Zambia tovuti Zambia Watchdog iliandika Jumatatu ikiwa na kichwa cha habari “Mike Tyson afanya mabadiliko ya kijinsia katika upasuaji uliofanikiwa”. Lakini ‘link’ hiyo kwa sasa inasema ukurasa hauwezi kufunguka.
Mr O’Farrell anasema hadithi ya awali ilipelekwa katika bodi ya waandishi wa NewsBiscuit na baadae timu ya mtandao huo ikaweka picha juu yake na kuichapa katika ukurasa wao wa mbele Novemba 30.
“Hii si mara ya kwanza kwa makala NewsBiscuit kuchukuliwa kwa uzito wa juu barani Afrika” anasema.
Katika mwaka 2007, ilitengeneza hadithi ya kizushi kuhusu Rais wa zamani wa Ghana, John Kufor na kumletea mtafaruku kwa waandishi wa nchini mwake.
Habari hii ya NewsBiscuit ambayo haina ukweli wowote, ikiwa imelengwa mahsusi ‘kupasua’ vichwa vya watu, imekuwa kama sikukuu ya wajinga kwa Watanzania ambapo vyombo vingi vya habari pamoja na mitandao ya kijamii viliingia mkenge na kuitumia habari hiyo.Chanzo:www.saluti5.com
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s