Kutoka IKULU Zanzibar:Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Azindua Sensa Ya Miti

 
 

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipima mti kujua upana wake baada ya kuzindua zoezi la sensa ya miti (woody Biomass Survey) katika hifadhi ya Taifa ya msitu wa Jozani jana,(kulia) Naibu waziri wa Kilimo na Maliasili Mtumwa Kheir Mbaraka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Affani Othman Maalim,(kulia).Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, 
Ikulu-ZanzibarWIZARA ya Kilimo na Maliasili na Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu, Baraza la Mainispaa Zanzibar, Mabaraza ya miji Pemba na Hamlashauri zote za Wilaya zimetakiwa kushirikiana katika kuimarisha mazingira kwa kupanda miti katika barabara za mijini na vijijini kwa Unguja na Pemba. Kauli hiyom imetolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa sensa ya miti Zanzibar, hafla iliyofanyika huko Jozani Mkoa wa Kusini Unguja. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Srikali iko tayari kutoa msukumo na kuhakikisha kwamba lengo hilo linafanikiwa kwa wakati na kusisitiza haja ya kutunzwa na kudumisha miti hiyo. Alisema kuwa sensa ya miti ni muhimus ana katika kupanga mipango ya maendeleo na kueleza kuwa kukamilika kwa kazi hiyo kutawezesha kupatikana takwimu muhimu na kuelewa wingi, ubora na aina za miti ya misitu, viungo na matunda iliyopo Zanzibar.

 
 
“Tunahitaji kuwa na takwimu sahihi za sasa ili tuweze kupanga mikakati bora na mipango mikakati bora na mipango muhimu ya maendeleo, hasa katika kuidhibiti misitu na miti iliyopo na kujipanga katika kuongeza mingine”, alisema Dk. Shein. Aidha, Dk. Shein alisema kuwa zoezi hilo litahusisha miti ya misitu, matunda na biashara ikiwemo karafuu hivyo, kukamilika kwa kazi ya sensa ya miti itawezesha kuzifahamu takwimu muhimu za zao hilo ikiwemo wingi, umri, urefu wa mikarafuu na maeneo yenye mikarafuu. Dk. Shein alitoa changamoto kwa Wizara ya Kilimo na Maliasili kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko zitumie matokeo ya utafiti wa upimaji wa miti ili kuyaondosha matatizo yaliopo na hatimae Zanzibar iweze kurudi katika biashara yake ya kuuza matunda nje ya nchi hasa Dubai kama ilivyokuwa hapo kabla. 
 
  Alisema kuwa takwimu zitakazotokana na kazi hii ya sensa ya miti ni muhimu na zitasaidia pia, katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni agenda muhimu kitaifa na kimataifa. Alisisistiza kuwa umuhimu huo unaonekana hasa katika nchi za visiwa kama Zanzibar ambapo kama hatua za mapema hazikuchukuliwa athrai kubwa kwa jamii kiuchumi na kimazingira zinaweza kutokeza. Dk. Shein alirejea wito wake wa kuwataka wananchi wasikate miti ovyo ikiwemo minazi na miti mengine ya matunda na misitu.  
 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kwa kutoa shukurani maalumu kwa washirika wa maendeleo ikiwemo Serikali ya Norway kupitia Ubalozi wake uliopo nchini kwa kuunga mkono na kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zake za kufanikisha utekelezaji wa mradi wa sensa ya miti Zanzibar. 
 
  “Leo ni siku muhimu katika utekelezaji wa azma yetu ya kuwa na usimamizi bora wa maliasi za misitu, matunda na viungo. Maliasili hizi ni muhimu kwa uchumi wetu, kwa utunzaji wa mazingira na kwa maendeleo ya jamii kwa sisi tuliopo na vizazi vijavyo”, alisisitiza Dk. Shein. Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar imejaaliwa kuwa na rasilimali muhimu ambazo zipo baadhi ya nchi hazina ikiwemo uzuri wa mazingira ya kijani kutokana na hali ya hewa, miongo inayopishana, mvua za wastani, wastani wa jua nakuwepo wka rasilimali zikiwemo za bahari na fukwe zake, misitu ya asili na wanyama ambao wako Zanzibar tu. 
 
  Hakuacha kusisitiza kuwa watu wasisahau kuwa nishati inayotumika sana ya kuni inatokana na misitu ambapo takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wa Zanzibar wanatumia nishati hiyo katika matumizi ya kila siku hasa kwa kupikia, hivyo matumizi endelevu ya nishati hiyo ni muhimu hivi sasa na vizazi vijavyo. Katika uzinduzi huo, Dk. Shein alianza kwa kukata utepe kwa kuashirikia uzinduzi huo akiambatana na Balozi wa Norywa nchini Tanzania na hatimae kufanya zoezi la kupima miti akiwa mtu wa mwanzo na baadae kupanda miti yeye pamoja na viongozi wakuu waliohudhuria katika uzinduzi huo akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd.  
 
Pia, alitoa shukurani wka serikali ya Finland ambayo nayo imeunga mkono juhudi hizo kupitia mradi wa SMOLE ambao walitoa fedha kwa matayarisho ya awali. Mapema wananchi wa maeneo hayo katika risala yao walieleza kuwa kuwa hivi sasa jamii tayari imeshaelewa umuhimu wa uhifadhi na hasa uhifadhi ambao unakwenda sawa na maendeleo yao. Hivyo wameanza kupata taaluma za kuanzisha midogo midogo ikiwemo ya ufugaji wa nyuki, kujuhusisha na utalii wa mazingira na nyenginezo. Nae Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Bakari Asedi alisema kuwa senza hiyo ni ya pili kufanyika hapa nchini ambapo sensa ya mwanzo ya kuhesabu miti ilifanyika kwa 1997, ambapo iligundulika kuwa kila mwaka miti 1000 hukatwa. 
 
  Na 
Rajab Mkasaba, 
Ikulu-Zanzibar
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s