Na gazeti la Mwananchi: ODM Kenya yamkingia kifua Magufuli

   
CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) cha Kenya, kimezungumzia uamuzi wake wa kumwalika Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni nchini humo, uliozua mjadala mkubwa nchini.
 
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
 
Desemba 7 mwaka huu, chama hicho cha upinzani nchini Kenya kilimwalika Dk Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja vya Kasarani ambako pamoja na mambo mengine, alimpigia debe Raila Odinga ili achaguliwe kuwa Rais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
 
Hatua hiyo ya Dk Magufuli ilizua mjadala mkubwa, huku Chadema kikidai kuwa ni makosa kwa nchi moja kuingilia siasa za nchi nyingine na kumtaka waziri huyo aeleze kama alitumwa na Serikali au la.
 
Chadema pia kilimtaka Rais Jakaya Kikwete atolee kauli hatua hiyo ya waziri wake, vinginevyo nchi itakuwa na uhusiano mbaya na Kenya, endapo Raila hatachaguliwa kuwa Rais.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa ODM, Profesa Peter Anyang’Nyong’ alisema hakuna haja ya Watanzania kumzonga Waziri Magufuli, kwani ujio wake Kenya, ulitokana na mwaliko wa Odinga.
 
Profesa Anyang’Nyong’ ambaye chama chake cha ODM kilitangaza kuungana na chama kingine cha Wiper Democratic cha Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka katika uchaguzi huo alisema Odinga alimwalika Magufuli kama rafiki yake wa muda mrefu na rafiki wa ODM.
 
“Waziri Mkuu wetu Odinga ndiye aliyemwalika Magufuli na alimwalika kama rafiki yake wa karibu. Kuja kwake huku (Kenya) kulikuwa safari binafsi. Hakukuwa (kuja) na uhusiano wowote na wadhifa alio nao Tanzania,” alisema Profesa Onyang’Nyong’.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s