WAZIRI MKUU AAHIDI TREKTA KWA VIJANA WA ILUNDE

 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kutoa trekta moja kwa ajili yakikundi cha vijana katika kata ya Ilunde ili waweze kuondokana na

kilimo cha jembe la mkono na waboreshe uchumi wa eneo hilo.

Ametoa ahadi hiyo leo (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Ilunde kwenye uwanja wa shule ya msingi Ilunde
katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele,
mkoani Katavi.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Katavi alisema atawapatia
trekta hilo kama mkopo ili nao wakirudisha trekta jingine, liweze
kukopeshwa kwa kikundi kingine. “Hapa naanzisha ‘Kopa trekta lipa
trekta’. Litakuja likiwa na jembe lake pamoja na harrow,” alisema
Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

“Ni lazima tuondokane na kilimo cha jembe la mkono kwa sababu hakina
tija… na zaidi nasisistiza kuondokana na kilimo cha matuta kwa
sababu kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo
lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alielezwa matatizo yanayowakabili wakazi hao yakiwemo
ubovu wa barabara ya kutoka Inyonga (km. 60) na ukosefu wa wauguzi wa
kike kwa ajili ya akinamama wajawazito. Pia waliomba kupatiwa minara
wa mawasiliano ya simu kwa sababu wanapotaka kupiga simu, wanalazimika
kupanda mti mmoja tu ambao uko km.12 kutoka kijijini hapo.

Akijibu maombi yao, Waziri Mkuu aliwaita Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda na Mhandisi wa Wilaya hiyo ili watoe maelezo kwa wananchi hao.
Kuhusu wauguzi, mganga mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Emmanuel Kamgobe
alisema wanashugulikia suala hilo.

Continue reading →

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s