Rais Jakaya Kikwete Aipa Vyombo Vipya na Vya Kisasa bendi ya muziki wa dansi ya Vijana Jazz, ‘ Wana Air pambamoto’

 

 Wana wa Vijana Jazz wakiwa kazini, Kulia ni, Saburi Athumani (Kiongozi wa bendi), Abdallah Mgona Hazelu (Katibu wa bendi), Nuru Mhina ‘Baby Whiye’ na Roshi Mselela, wakiimba ukumbi wa Masae Bar, Kawe.

NA BASHIR NKOROMO.
BAADA ya kuwa ‘juu ya mawe’ kwa muda mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya  Vijana Jazz,  ‘ Wana Air pambamoto’ imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa imeipua vibao viwili vipya  kusuuza nyoyo za mashaki wake.
 
Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni jijini Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha kwamba mashabiki wake wengi bado wapo.
 
Kwenye ukumbi huo unaotazamana na kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packes, Vijana Jazz ilithihirisha kuwa ‘bado wamo’, kwa kupiga nyimbo zake za zamani zikiwemo ‘Mary Maria’, ‘Mwsiho wa mwezi’, ‘Ngapulila’ na ‘mawifi’, zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo,  marehemu Ahmed Maneti katika miaka ya 1980.
 
Nyimbo hizo ziliwafanya mashabiki wa bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba sambamba na wanamuziki waliovyokuwa wakiimba jukwaani na wengine kwenda jukwaani kutuza waimbaji.
 
Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri,  wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.
 
Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua ni  ‘Utanieleza nini’, utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza  uliotungwa na Mgonahazelu.
 
Athumani alisema, nyimbo hizo zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.
 
Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo hizo kwa ajili ya kiusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi imo katika jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.
 
“Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa Kikweye. Kwa kweli tunamshukuru sana”, alisema Mgoma Hazeru wakati kabla ya bendi hiyo kuanza kuimba wimbo wao mpya wa ‘Utanieleza nini’.
 
Vijana Jazz ni moja ya bendi ambazo Mratibu wa Budurani zote kwenye ukumbi huo wa Masae, Juma Mbizo, amesema atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama Msondo Band na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s