WILAYA YA MLELE KUWA NA HALMASHAURI MBILI – WAZIRI MKUU

 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi
itakuwa na Halmashauri mbili za Mlele na Nsimbo ili kurahisisha utoaji
huduma kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo janamchana (Jumamosi, Desemba 15, 2012), wakati
akizungumza na wakazi wa kata ya Inyonga kwenye viwanja vya shule ya
msingi Inyonga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake jimboni kwake
Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Aliwaeleza wakazi hao kwamba Rais Jakaya Kikwete aliamua kuwapa wilaya
mpya na mkoa mpya kwa ili kuleta maendeleo kwa haraka. “Rais Kikwete
alifanya hivyo kwa sababu alijua kwamba rasilmali zikiletwa Rukwa
(mkoa wa zamani) hadi zifike hapa Mlele zitakuwa ni kidogo sana,”
alisema.

Kufuatia mgawanyo huo, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele itakuwa na kata
13 ambazo ni Ilunde, Ilela, Nsenkwa, Inyonga, Utende, Kasanga na
Mamba. Nyingine ni Majimoto, Mwamapuli, Mbede, Usevya, Itenka na
Kibaoni.

Nayo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo itakuwa na kata 11 ambazo ni
Ugalla, Uruira, Kasokola, Mtapenda, Nsimbo na Sitalike. Nyingine ni
Kapalala, Machimboni, Litapunga, Itenka na Magamba.

Ili kuendana na kasi ya mabadiliko, Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao
wachangamkie fursa zilizopo kwa kuachana na kilimo cha matuta.
Aliwataka mabwana shamba waandae mashamba-darasa kwa kila kijiji ili
wananchi waweze kujifunza kwa mifano.
Continue reading →

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s