Mhe.Pinda amtimua Mkandarasi wa bandari za Ziwa Tanganyika

 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kumfukuza kazi mara moja mkandarasi anayejenga bandari ndogo nne katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika.

Prime Minister Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Bandari hizo zinajengwa katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi. Pinda anataka TPA imfukuze kazi mkandarasi huyo baada ya kushindwa kuikamilisha kwa zaidi ya miaka miwili.

Mkandarasi huyo, Kampuni ya Modspan Enter Limited ya Dar es Salaam ilishinda zabuni ya kujenga bandari ndogo za Kipili wilayani Nkasi (Rukwa) na Karema (Katavi) na bandari za Lagosa na Sibwesa mkoani Kigoma zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Waziri Mkuu alisema mkandarasi huyo amekosa uwezo wa kuimudu kazi hiyo. Alitoa agizo hilo mjini Mpanda baada ya kuarifiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk Rajab Rutengwe kuwa mkoa huo hauna bandari ya kisasa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.

Waziri Mkuu alifahamishwa pia kuwa pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kuanza kujenga bandari kijijini Karema, lakini kwa sasa ujenzi umesimama baada ya mkandarasi kushindwa kuimudu kazi kwa kukosa uwezo.

Kama bandari hiyo ingekamilika, ingefungua soko kubwa la bidhaa mbalimbali katika nchi jirani na kuvutia wawekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika wenye mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi.

Kutokana na maelekezo hayo, Pinda alishangazwa na kuhoji iweje mkandarasi mwenye uwezo huo mdogo ambaye ameshindwa kuimudu kazi hiyo ashinde zabuni za kujenga bandari tatu za Kipili, Karema na Sibwesa katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s