Na gazeti la Mwananchi: Kigogo NCCR-Mageuzi ahamia Chadema

 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbess Lema akipeana mkono na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara na Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara ambaye jana alitangaza kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema mjini Babati jana. Picha na Joseph Lyimo
 
Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
 
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga. Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.
 
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.
 
Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.
 
“Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo,” alisema Tara.
 
Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s