Kampuni ya Prime Time Promotions yatoa milioni 105 kufanikisha shamra shamra za mkutano mkuu wa Yanga

 

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni 105 kwa uongozi wa timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wao mkuu pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. 
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga na Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga wakikabidhiana mikataba yao ya makubaliano ya kikazi.
 Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akitiliana saini ya makubaliano na club ya Yanga kuhusiana na makubaliano ya timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Ltd,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akifurahia jambo na baadhi ya Wanahabari mara baada ya kutiliana saini mikataba yao ya kikazi na Club ya Yanga,uliofanyika mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi za club hiyo,Jangwani jijiini Dar
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga akizungumza machache kuhusiana na makubaliano yao ya kikazi na Club ya Yanga ikiwemo sambamba na makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 105 yaliyotolewa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa Club ya Yanga,Clement Sanga akizungumza mapema leo kwenye makao makuu ya timu hiyo na Waandishi wa habari kuhusiana na timu ya Yanga  kusaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Primetime Promotions Lt,ambapo Prime Time Promotions imekubali majukumu ya matayarisho yote ya mkutano wa wanachama wote wa Yanga
uliopangwa kufanyika Januari 19 2013.Kushoto ni katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na kulia ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Joseph Kusaga.

Aidha katika mkutano huo imeelezwa kuwa matayarisho hayo yatahusisha ukumbi na viambatanisho vyote
muhimu,ikiwemo Live TV coverage na matangazo mbalimbali ya kuhamasisha mafanikio ya mkutano.

Aidha katika kuongeza mapato kwa maendeleo ya club na matayarisho ya kumalizia ligi, Prime Time Promotions Ltd,imetoa milioni 105 mapato ya uhakika kwa timu ya Yanga na Prime Time Promotions  itaandaa mechi ya kirafiki

ya kimataifa katika kukamilisha shamrashamra za kusindikiza mkutano huo wa
kwanza wa uwazi wa kihistoria kwa Club ya Yanga. Habari Picha na Michuzijr Blog.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s