TAZAMA WADAU WA SKYLIGHT BAND WANAVYOSAKATA NGOMA THAI VILLAGE…!


 

Ijumaa huwa pana changamka mno ndani ya kiwanja cha Thai Village ambapo bendi ya Skylight hufanya mambo kibingwa kwa kuima traki za mbele na za kwao wenyewe , hapa sasa , watu wamejimwaga kwenye sakafu na wamejiachia kinoma noma! Mlangoni kupenya ni shilingi elfu tano (5000)   .Pia unaweza kuzama…http://Wwwmasterkif.blogspot.com

Advertisements

NAPE ashiriki ujenzi wa madarasa kasulu


 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye leo ameshiriki katika shughuli za ujenzi wa madarsa katika Shule ya Sekondari Nyasha Wilayani Kasulu.
 
Miongoni mwa Shughuli hizo alizoshiriki ni pamoja na kuunganisha kenchi, kubeba mawe na kupiga ripu chumba kimoja wapo cha madarasa na kumalizia na kupanda mti katika uwanja wa shule hiyo.
 
Nape Nnauye akisaidiana na mafundi katika ubebaji wa jiwe  la ujenzi wa madarsa katika Shule ya Sekondari Nyasha Wilayani Kasulu.

  
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha CCM Nape Nnauye akichapa  kazi ya ujenzi wa madarasa kasulu
Picha zaidi tembelea FatherKidebu.blog 

MGOGORO WA GESI MTWARA:Pinda azima uasi


 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi watakavyonufaika na gesi itakayozalishwa mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda
 
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga mpango wa kusafirisha gesi hiyo.
 
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
 
“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu… kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema Pinda na kuongeza:
 
“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme… tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”
 
“Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi viwanda vije… nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu. Nikawauliza wataalamu wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa wapi, wakanijibu Madimba… nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza vya kutosha wananchi suala la gesi.” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa makofi… “Nafikiri tatizo ni sisi Serikali hatukuwa na mpango mzuri wa kuwaelimisha wananchi.”
 

LULU APATA DHAMANA


 

 Elizabeth Michael (Lulu) 
MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.

Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.Chanzo:hakingowiblog

 

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aung’uruma Kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Addis Ababa


 
Rais  Jakaya Mrisho  Kikwete akihutubua  mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Jakaya Mrisho  Kikwete  na ujumbwe wake akitoka nje ya ukumbi baada ya kuhutubua  mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa nane toka kulia, akiwa na viongozi wenzake katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa leo Januari 27, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.Picha na IKULU