WATANZANIA SASA WAFIKIA MILIONI 44.9

 

 

 

Watanzania wameongezeka kwa kasi tangu mwaka 1967 ambapo walikuwa 12,313,054 na sasa wako 44,929,002.
 
 
Hatua hiyo imemshitua Rais Jakaya Kikwete ambaye amesema idadi hiyo inaweza kuwa mzigo mkubwa kwa Taifa, jamii na uchumi wa nchi katika kuwahudumia na kukidhi mahitaji yao ya msingi.
 
“Lazima tuwe na mipango madhubuti ya kiuchumi ili idadi hii ya watu iweze kuhudumiwa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza: “Idadi hii ni kubwa na naomba familia zingatieni uzazi wa mpango, vinginevyo hali ya maisha itashuka kwani ushindani utakuwa mkubwa wa kupata huduma wakati raslimali zilizopo ni ndogo na hazitoshelezi idadi hiyo.”
 
Matokeo ya Sensa iliyofanyika Agosti 26 mwaka jana yanaonesha kuwa idadi ya Watanzania kwa sasa ni milioni 44.9 na ifikapo mwaka 2016 itaongezeka hadi watu milioni 51.
 
Matokeo ya Sensa hiyo ambayo ni ya tano kufanyika nchini, yalitangazwa jana na Rais Kikwete ambaye alionesha kushitushwa na kasi kubwa ya ongezeko la watu nchini hadi akatoa mwito kwa Watanzania kuzingatia uzazi wa mpango.
 
Katika takwimu hizo ambazo zinaonesha kuwa jumla ya Watanzania ni 44,929,002 kati yao idadi ya watu Tanzania Bara ni 43,629.434 na Zanzibar idadi yao ni 1,303,568.
 
Mwaka 1967 ambako sensa ya kwanza ilifanyika wakati Tanzania ikiwa Jamhuri ya Muungano, Watanzania walikuwa 12,313,054 kati yao Bara walikuwa 11,958,954 na Zanzibar 354,400.
 
Sensa ya mwaka huu ilifanyika baada ya miaka 45 ya sensa ya kwanza kufanyika na ongezeko la Watanzania kwa kipindi hicho ni watu milioni 33.
 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s