TAARIFA RASMI KUTOKA EWURA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO MPYA ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO,TAREHE 2 JANUARI 2013 HIZI HAPA

 
   Mkurugenzi Mkuu wa EWURA.Haruna Masebu
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI  KUANZIA JUMATANO, TAREHE 2 JANUARI 2013
 
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  inatangaza  bei kikomo za 
bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, 
Tarehe 2 Januari 2013.Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli 
nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo.
 
 
(a)    Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 05 Desemba 2012. Katika toleo hili, bei za rejareja kwa  Petroli,  Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 126/lita sawa na asilimia 5.96; Dizeli Sh 32/lita sawa na asilimia 1.60; na Mafuta ya Taa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.50. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo  haya  mawili zimepungua kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 126.10/lita sawa na asilimia 6.17; Dizeli kwa Sh 32.48/lita sawa na asilimia 1.69; na Mafuta ya Taa kwa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.6. Mabadiliko haya ya bei yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani. 
 
 
(b)            Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
 
 
(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011. 
 
 
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
 
 
(e)Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.
 
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s