MAFANIKIO ZAIDI KUPATIKANA ZANZIBAR ENDAPO WANANCHI WATADUMISHA MSHIKAMANO

 

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar    

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema mafanikio yote yaliyopatikana Zanzibar katika kipindi cha miaka 49 na miaka ijayo kwenye nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa msingi wake mkubwa ni Mapinduzi ya Januari 1964.

 Amesema mafanikio zaidi yatapatikana iwapo Wananchi wataendelea kudumisha mshikamano na amani iliyopo Zanzibar pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo Zanzibar.

 Rais Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akilihutubia Taifa katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

 Amesema ushirikaiano wa Serikali na wananchi umeipatia Zanzibar mafanikio mazuri katika kuimarisha uchumi wake ambao mwenendo wake umeliwezesha pato la Taifa kufikia Shilingi Bilioni 1,198 mwaka 2012 kutoka Bilioni 946 mwaka 2011.

 Amefahamisha kuwa mafanikio hayo yametokana na kukua kwa Sekta ya Uvuvi, Biashara na ujenzi wa Mahoteli na Mikahawa jambo ambalo limesaidia Serikali kupunguza mfumko wa bei kutoka asilimia 20 mwaka 2011 hadi asilimia 4.2 mwaka 2012.

 Kuhusu Kilimo Rais Shein amesema Serikali yake inaendelea kuchukua juhudi mbali mbali za kukiendeleza kilimo ikiwemo kuimarisha Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili kuhakikisha kuwa Hekta 8,521 za Unguja na Pemba zinatumika kwa ajili ya kilimo hicho.

 Aidha ameongeza kuwa Serkali inaendelea na azma yake ya kulinda hadhi ya zao la Karafuu ambapo mkakati wa kupatikana kwa Utambulisho maalum wa Karafuu za Zanzibar (Branding) upo katika hatua nzuri.

Continue reading →

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s