Na Gazeti la Mwananchi: Wadau wataka Kiswahili Chuo Kikuu

 

 
Na Waandishi Wetu
 
JUKWAA la Taasisi na Mamlaka zinazosimamia na kudhibiti ubora wa elimu nchini, limependekeza kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu.
 
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Sinare Maajar akizindua hivi karibuni mradi maalum wa kozi za kiswahili zitakazofundishwa katika Chuo kikuu cha Indiana nchini Marekani.

Jukwaa hilo linaundwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza za Mitihani la Taifa (Necta), Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

 
Lilitoa mapendekezo hayo jana wakati likiwasilisha maoni yake kwa tume hiyo jijini Dar es Salaam, huku likitaka pia Wizara ya Elimu igawanywe ili kuwe na mamlaka mbili ambazo ni Wizara ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Utamaduni na Wizara ya Elimu ya Ufundi na Elimu ya Juu.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Profesa Sifuni Mchome alisema kwamba wamependekeza Kiswahili kitumike kufundishia kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu, ili kuweza kukuza kiwango cha elimu nchini.
 
Profesa Mchome alisema kabla ya kuanza kutumika kama lugha ya kufundishia, lugha hiyo iandaliwe kitaalamu ili kuhakikisha inagusa ngazi zote za masomo ambayo yatafundishwa katika taasisi za elimu.
 
“Tumetaka lugha ya Kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ili kuhakikisha tunakuza lugha yetu.” alisema Profesa Mchome na kuongeza;
 
“Tunataka Katiba Mpya itamke kwamba kutakuwa na mipango sahihi kabla ya kuanza kutumika kwa lugha hiyo ya kufundishia ili kuhakikisha inagusa maeneo yote.”
 
Profesa Mchome alisisitiza kwamba wamependekeza pia Katiba Mpya itamke kwamba elimu ya msingi itakuwa haki kwa kila raia wa Tanzania na itapatikana bure bila gharama yoyote.
 
“Tumependekeza elimu ya msingi iwe bure kwa kila raia wa Tanzania na ipatikane bila gharama yoyote wala michango na kwamba gharama zote zitoke serikalini,” alisema.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s