EMMANUEL OKWI:Simba imeniuza dola 300,000 hivyo nakwenda Etoile du Sahel ya Tunisia

Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba ile ishu ya mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman imefikia mwisho.
Taarifa za ndani kutoka Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya dola za kimarekani laki tatu.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.
“Ni kweli Mwenyekiti yupo Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel, ada ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya.” – kilisema chanzo cha habari kutoka Simba.
Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF, shaffih anapatikana kwenye shaffihdauda.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s