Jeshi la Polisi linahitaji mapinduzi makubwa

 

 NI kwamba Jeshi la Polisi nchini linahitaji mapinduzi makubwa ili kulirejeshea imani kwa wananchi na hatimaye kufanikisha mkakati wake wa ulinzi shirikishi.
 
 
Daniel Mjema
Matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya vyama vya siasa, ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, matumizi holela ya silaha za moto, kushiriki uporaji, ujangili na matendo mengine mabaya kumechangia kuongezeka kwa chuki kati ya polisi na wananchi.
 
Miaka ya nyuma hatukuwahi kushuhudia matukio ya kutisha ya wananchi kuua polisi hadharani, lakini sasa polisi wetu wanauawa na raia. Hii si hali ya kawaida hata kidogo, na haitakiwi kuachwa iendelee kwani inaweza kuleta madhara makubwa.
 
Katika makala yangu moja niliwahi kusema hapa kwamba ‘tusiwakomaze wananchi wetu kwa risasi na mabomu’. Niliyasema hayo nikitazama namna uhusiano kati ya polisi na raia ulivyokuwa unazidi kuyumba. Jeshi la Polisi linalalamikiwa kutumika zaidi kisiasa na kutofanya kazi kwa weledi. Kanuni zinakataza polisi kushabikia chama chochote cha siasa lakini matendo yao ni kinyume na dhana hiyo.
 
Ipo mifano mingi tu kuthibitisha kuwa kwa baadhi ya mazingira, polisi wetu wamekuwa wakidaiwa kutekeleza wajibu wao kwa kuipendelea CCM ama kwa kujua au kwa kushawishiwa na ‘wenye nchi’ kufanya hivyo.
 
Mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi ni matokeo ya polisi kufanya kazi zao kwa double standard (upendeleo) na kuvikandamiza vyama vya upinzani.
 
Polisi walipopiga marufuku mikutano ya Chadema kwa kisingizio cha Sensa papo hapo kuruhusu mikutano ya ndani ya CCM na ile ya kampeni Zanzibar hakika hapa jeshi letu lilionyesha upungufu mkubwa wa weledi.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s