Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba alazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU)Hospitali ya Aga Khan

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba  
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga Khan lakini akasema kuwa hadi jana jioni, hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri.Kwa Habari zaidi bofya na Endelea……>>>>>
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s