Shaaban Lamania hatunaie tena Duniani

 

 
Hayati Shaaban Lamania,enzi za 
uhai wake!
Inna lillaahi wa inna ilayhi raji’oon
 
MKURUGENZI Mipango na mtunzi mkubwa wa nyimbo za kundi kongwe la East African Melody, Shaaban Lamania , amefariki alfajiri ya kuamkia jana.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa fedha wa kundi hilo, Ashraf Mohamed, msiba uko Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam.
 
Ashraf amesema mipango ya mazishi inaendelea na watatoa taarifa baadae kuhusu muda na siku ya mazishi.
 
Lamania ambaye amekuwa nje ya jukwaa kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kupooza, atakumbukwa kwa tungo zake nyingi ambazo hadi leo hii bado zinaendelea kulibeba kundi la Melody.
 
Miongoni mwa tungo zake kali ni pamoja na “Utalijua jiji” na “Mwanamke khulka”.
 
Mbali na utunzi, Lamania pia alikuwa mpigaji mahiri wa gitaa la solo.
‘Hakika sisi ni wa Mungu na kwake ni marejeo’.

M/Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Ameen

Advertisements

One Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s