Dk Willbroad Slaa Afungua Kongamano la Viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chadema(CHASO) Nakusema:“Inakuwaje polisi wanawapiga mabomu wanafunzi wanaofanya maandamano, lakini wanashindwa kuzuia Twiga wanaotoroshwa nje ya nchi, tuungane, tushirikiane na tupige kelele, ili mali zetu zirudi,”

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa akiongozana na viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama hicho (CHASO) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililofanyika katika Ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix 
 —
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema kuwa kuanzia mwaka huu hadi 2015, chama chake kitaipeleka mchakamchaka CCM, kwa kuwa chama chake kimefanikiwa kuwaamsha Watanzania.
Alisema kwamba Watanzania sasa wameamka na kutambua utajiri wa nchi yao na jinsi   rasilimali zinavyotoroshwa nje ya nchi na kuanza kudai kufaidika nazo kwa nguvu. Hivyo Chadema kitaitumia fursa hiyo kuipeleka puta CCM, lengo likiwa kuhakikisha kila Mtanzania anaishi maisha bora.
Dk Slaa alisema hayo alipokuwa akizungumza katika kongamano la Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini, ambao ni wafuasi wa chama hicho (CHASO), lililofanyika Dar es Salaam jana.

Alieleza kuwa kinachotokea mikoa ya Lindi na Mtwara, pamoja na maandamano ya hivi karibuni ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ni majibu tosha kwa CCM, kwamba mikutano ya Chadema iliyofanyika mikoa mbalimbali nchini imewaamsha wananchi.
Wanafunzi zaidi ya 500 walihudhuria kongamano hilo kutoka  IFM, Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na  Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), pamoja na vyuo mbalimbali vilivyopo Dar es Salaam na mikoani.Kwa habari Zaidi Bofya na Endelea……….>>>>>>>
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s