MAWAZIRI WABAINI KUONDOLEWA KWA KIPENGELE CHA MKATABA

 

DK-HARRISON-MWAKYEMBEMAWAZIRI wanne wamebaini kuondolewa kipengele ndani ya mkataba kinachomtaka mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya Leinton ya Singapore kuiachia Mamlaka ya Bandari (TPA) vifaa vyenye thamani ya sh bilioni 3 baada ya kumaliza ujenzi.

Mkandarasi huyo ambaye amemaliza ujenzi wa mtambo wa mafuta bandarini, alitakiwa kuviacha vifaa hivyo.

Mawaziri waliobaini kuondolewa kwa kipengele hicho kilichokuwepo ndani ya mkataba, ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda;  Waziri wa Fedha na Uchumi, Wiliam Mgimwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Hayo yalibainika jana baada ya mawaziri hao kufanya ziara bandarini na kupata taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande.
Akizungumza na wafanyakazi wa bandari, Dk. Mwakyembe alisema wamefanya ziara hiyo ya kawaida ya kutembelea chombo hicho muhimu katika kukuza uchumi wa taifa.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s