Mgogoro wa gesi Mtwara unanifedhehesha; Mh Mkapa.

 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea kufedheheshwa kwake na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na mihadhara.
Mkapa alitaka wakazi hao kuacha kulumbana na Serikali kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta mwafaka kwa njia ya amani.

Katika tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana, Mkapa alisema: “Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti ya maendeleo.

“Nikiwa kama mwana – Mtwara na raia mwema, mpenda nchi, nimefedheheshwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara, kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara.

“Badala yake wajipange kukaa pamoja katika meza moja,  kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake, hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo. Liwezekanalo leo lisingoje kesho.”

Mkapa alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi wa Serikali.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyalaani maandamano hayo akisema walioyaandaa wamelenga kuigawa nchi vipandevipande, Chadema kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kumbana waziri huyo ili aondoe udhaifu uliopo katika sekta ya nishati.

 “Walioratibu maandamano hayo ni watu hatari kwelikweli kwa amani na usalama wa Tanzania, wanataka kuigawa nchi vipandevipande, hawaitakii mema nchi yetu kwa utulivu na amani tuliyonayo,” alisema Profesa Muhongo.
Wananchi hao wamekuwa wakiitaka Serikali kufanya uzalishaji wa gesi hiyo mkoani humo ili kuweza kuinua maendeleo ambayo yamepotea katika ukanda huo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s