YALIYOJIRI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA YANGA JANA, SENDEU, MWESIGWA WAFUTIWA UANACHAMA

Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans, Yusuf Manji akifafanua baadhi ya mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo, maendeleo ya Klabu hiyo pamoja na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar, Sahihisho la katiba yao, masuala mbalimbali yanayohusiana na wanachama wao, ustawi wa wanachama wao, mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mengi yaliyoongelewa.
 Baadhi ya wanachama wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, kutoka maeneo mbalimbali, wakitawanyika nje ya ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jana mchana mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa Mwaka, ambao umefanikiwa na kuweza kufanya mabadiliko katika baadhi ya maeneo ya nafasi za uongozi, ambapo aliyekuwa Ofisa Habari wake, Louis Sendeu na aliyekuwa Katibu Mkuu, Selestine Mwesigwa, wamefutiwa Kadi zao za uanachama, kwa kile kilichoelezwa kuwa mwezi Septemba, mwaka jana walitinga Mahakamani kupinga kufukuzwa kazi katika Klabu hiyo.


Katika suala hilo la Kimahakama, Mwesigwa aliishitaki Klabu ya Yanga akiidai kiasi cha Sh. 183,400,050, huku Sendeu akidai kiasi cah Sh. 79, 900,050, ambapo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, aliwahoji wanachama, juu ya hilo na kupata jibu la pamoja kutoka kwa wanachama waliosema kwa pamoja kuwa, ”Wavuliwe uanachama kwa kukosa uzalendo na Klabu yao”.Picha na habari kwa hisani ya Mussa Mateja
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s