Neno La Leo: Hata Kibogoyo Anaweza Kukuuma!

1 21de5

 

Ndugu zangu,

Nchi yetu inapita kwenye kipindi kigumu.  Kuna moto unafukuta, tumeshauona moshi mkubwa, ni ishara ya moto mkubwa. Tukikaa chini na kuitanguliza busara na hekima, basi, tuna nafasi ya kuizuia dhahma kubwa inayokuja. Na katika kuifanya kazi hii, bahati mbaya, muda si rafiki yetu. Muda unakwenda haraka.

Kibogyo ni binadamu asiye na meno. Hata hivyo, utafanya kosa kubwa kumdharau kibogoyo, kuwa hana uwezo wa kukudhuru kwa kutumia mdomo wake. Ukweli ni huu, kibogoyo akijawa na hasira, basi, anaweza kukuuma na hata  kukuachia alama mwilini.

 

 

Kuna hata wanadamu wenzako watakaokuuliza;

” E bwana, hii alama umeumwa na nini?”. Na ukweli lazima utajulikana, hata kama utajaribu kuuficha. Kuwa umetiwa adabu na kibogoyo!

Mnyonge mwogope hata katika unyonge wake. Mara nyingi huwa hana cha kupoteza. Ukimkandamiza sana. Basi,  hata katika unyonge wake, anaweza kukutemea sumu kali. Ni sawa na mjusi. Ni kiumbe mdogo, lakini, mjusi ukimwandama sana anaweza kugeuka nyoka. Atakudhuru.

Ndugu zangu,

Wanadamu tumeumbwa na mdomo mmoja, macho mawili na masikio mawili. Aliyetuumba alikuwa na maana yake; kuwa tusiongee sana, bali, tuangalie zaidi. Tusikilize zaidi. Na wa kuwaangalia na kuwasikiliza zaidi ni wanadamu wenzako,, bila ya kuwabagua.

Na kwa kiongozi, ni wale unaowaongoza. Hata kama miongoni mwao kuna vibogoyo.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s