
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.
Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).
Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.
Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
Chanzo Michuzi Blog
Advertisements
Registration bila faini kwa watahiniwa binafsi nikiwa na maana wale QT’S waliofanya mitihani yao 2012 wanaotakiwa kujisajili kwa ajili ya kufanya mitihani ya kidato cha nne 2013 ni tarehe 28.2.2013 baada ya hapo itakuwa ni ada pamoja na faini.swali matokeo yamechelewa hivi na kwa mtu aliye makini hawezi kujisajili pasipo kujua kwanza kama amefaulu kuendelea na kidato cha nne au kurudia mitihani ya QT! Je hamuoni kuwa hamuwatendei haki hao ndugu zetu?toeni matokeo mtu ajisajili akiwa ana uhakika.na je endapo atajisajili kabla ya matokeo na baada ya matokeo kutoka akakuta amefeli(QT Exams).je watarejeshewa hizo pesa zao? au ndo itakuwa imekula kwao!naomba nifahamisheni.
LikeLike
MATOKEO HADI LINI? MTUAMBIE.
LikeLike
tunaombeni mtuambie matokeo yatatoka lini ?????????????????????
LikeLike
Lini matokeo ya kidato cha nne(4) 2013 yatatoka?
LikeLike
Jamani tumechoka kusubiri
LikeLike