Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1 Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa
(a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67. Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.
(c) Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23 hawakufanya mtihani.
4.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a) Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.
(b) Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361.
5.0 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Idadi ya Wavulana
|
Idadi ya Wasichana
|
Jumla
|
|
I
|
1,073
|
568
|
1,641
|
II
|
4,456
|
1,997
|
6,453
|
III
|
10,813
|
4,613
|
15,426
|
I-III
|
16,342
|
7,178
|
23,520
|
IV
|
64,344
|
38,983
|
103,327
|
0
|
120,664
|
120,239
|
240,903
|
6.0 SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
ST. FRANCIS GIRLS
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS S.S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS S.S
|
69
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS S.S
|
88
|
PWANI
|
5
|
ROSMINI S S
|
78
|
TANGA
|
6
|
CANOSSA S.S
|
66
|
DAR ES SALAAM
|
7
|
JUDE MOSHONO S S
|
51
|
ARUSHA
|
8
|
ST. MARY’S MAZINDE JUU
|
83
|
TANGA
|
9
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
10
|
KIFUNGILO GIRLS S S
|
86
|
TANGA
|
11
|
FEZA GIRLS
|
49
|
DAR ES SALAAM
|
12
|
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
|
124
|
KILIMANJARO
|
13
|
DON BOSCO SEMINARY SS
|
43
|
IRINGA
|
14
|
ST.JOSEPH MILLENIUM
|
133
|
DAR ES SALAAM
|
15
|
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
|
64
|
KIGOMA
|
16
|
ST.JAMES SEMINARY SS
|
44
|
KILIMANJARO
|
17
|
MZUMBE SS
|
104
|
MOROGORO
|
18
|
KIBAHA SS
|
108
|
PWANI
|
19
|
NYEGEZI SEMINARY SS
|
68
|
MWANZA
|
20
|
TENGERU BOYS SS
|
76
|
ARUSHA
|
7.0 SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI S.S
|
40
|
LINDI
|
2
|
NDAME S.S
|
41
|
UNGUJA
|
3
|
MAMNDIMKONGO S.S
|
63
|
PWANI
|
4
|
CHITEKETE S.S
|
57
|
MTWARA
|
5
|
MAENDELEO S.S
|
103
|
DAR ES SALAAM
|
6
|
KWAMNDOLWA S.S
|
89
|
TANGA
|
7
|
UNGULU S.S
|
62
|
MOROGORO
|
8
|
KIKALE S.S
|
60
|
PWANI
|
9
|
NKUMBA S.S
|
152
|
TANGA
|
10
|
TONGONI S.S
|
56
|
TANGA
|
8.0 TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1 Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i) Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii) Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2 Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii) Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.
(iii) Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.
(iv) Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v) Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.
9.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a) Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
(b) Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
10.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOFUTWA
10.1 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.
Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:
S/N
|
AINA YA UDANGANYIFU
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
(i)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
|
04
|
(ii)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
|
170
|
(iii)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
|
590
|
(iv)
|
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
|
04
|
(v)
|
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
|
06
|
(vi)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
|
15
|
|
JUMLA
|
789
|
10.2 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao
(i) Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“Written responses to any examination question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“A candidate found to have committed an examination offence shall – (a) have his examination results nullified”
(ii) Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti) kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0 KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012
(a) Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
· www.udsm.edu.ac.tz, au
(b) Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
18 Februari 2013
KUPATA MATOKEO HAYO BOFYA HAPO CHINI
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012
We need something good 2get up our education. Too much feiler why! Waziri wa elimu kuwa mkali sana juu ya hili coz huku kwe2 singida mpaka leo hii kuna baadhi ya shule za sekondari bado hazijaanza kufundisha watoto wanaenda shule bure 2. Unategemea kidato cha pili uwachuje si watarudi wengi! Kama hawajahonga kwa wale wazazi wenye uwezo. Makapuku wanarudia. So kazia sana elimu imedropdown sana.
LikeLike
well thats so true , hope he works on that
LikeLike
Serikali iajili walimu wa kutosha katika shule zake zote
LikeLike
In general the Mnister of education can’t do this allon so I also say waziri wa elimu waamdie ao maofisa elimu wa mikoa wa kaze buti!
2013/2/20 kifltd
> ** > Joshua commented: “Serikali iajili walimu wa kutosha katika shule zake > zote”
LikeLike
wanafunzi inatupasa kua makini na masomo yetu!kwanini tufutiwe mitihani kwasababu ya kuandika matusi! we better get serious
LikeLike
NI KWELI SUALA LA ELIMU LAZIMA LITAZAMWE SANA,WAMEFELI WENGI SANA,HATA YALE MASOMO WALIOTEGEMEA PIA NAYO WAMEFELI!HATA YA DINI!
LikeLike
MR MTEGA ELIMU LIMEKUWA FUMBO KWETU MANA HALI MBAYAAAA
LikeLike
saaaaaaaana!
LikeLike
Jaman aibu kwa wale wote waliomalza 4m4 mwaka jana matoke co mazur mmefel sana yaan yanacktsha 2muombe yacje yakawakuta wengne!!!?
LikeLike
am real tired of this results an there is something is going on education sector.please do some thing on this…………………..it iz toooo much.
LikeLike
mm naichan sioni haja ya elimu kuwekwa kama mtu unatumia gharama then end of the day mtoto anashindwa kuendelea huo ni upumbavu mtupu sasa tuwape leke wapi hawa walio feli/
LikeLike
“upumbavu”maana yake nini?au na wewe hukufaulu mtihani wa lugha
LikeLike
ndugu zetu kma kuharibu wameshaharibu xo nikujipanga tu no way out
hata mtoto akikunyea mkono uckate kiganja
LikeLike
The government has harvested what they wanted.It’s preparing for the death of Tanzanian citizens.They should find the way to employ them.
LikeLike
tatizo kubwa hapa wakuu ni kuchanganya elimu na siasa !! hatufiki kwa mtindo huu
pili tusifanye elimu kuwa biasharaa!!!!!!!!! hatutatoboa kwa mtindo huu
LikeLike
serekali iliondoa mitihani ya kidato cha pili, waliofeli kimbilio ni
waalimu, mitaala haieleweki, mazingira ya kufundishia kwa ujumla ni mabovo kuliko. je nikitugani kitamfanya huyu mwanafunzi asifeli wakati “umimi kwanza” ndiyo umejaa TANZANIA.?naomba mnijibu tu.
LikeLike
mzee hapo umcchemka kweli kabisa jiuzutu baba.
LikeLike
lakini endelea kula mzee usijiuzulu mzee endelea kula watoto wetu wana fail 22222
LikeLike
ni jambo la kawaida xana wanafunzi kufeli mitihani lakini sio kwa mwaka huu? kutokana na hali hiyo inabidi ichukue hatua mbadala ili kunusuru maisha ya wanafunzi waliofeli mitihani hii! bila hivyo uhalifu utaongezeka kama zero zilivyo ongezeka kwenye matokeo!!!!!!!!!!!!!!
LikeLike
yatupasa kupeana moyo na kupanga” the next couse of action”.sikuzote majuto ni mjukuu, na maji yaksha mwagika hayazoleki.
kama pepa zinadunda .why dont you give it another try guys or study on samthing else .never stop tryn never loose hope!
LikeLike
Matokeo haya yataviathiri vyuo vikuu vyotd nchini maana ifikapo 2015 havitakuwa na wanafunzi wa kutosha kudahiliwa hata kama waliofaulu wote mtihani huu watafaulu pia mtihan wa form six 2015
LikeLike
nashukuru kauli ya serikali ya kusema kwamba turudie kusoma mwaka mzima na tufanye mtihani wa kidato cha nne naomba proposal hiyo ipitishwe ipasavyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
LikeLike
nilikuwa naomba serikali ifanye bidii ya kuwaongeza walimu pamoja na kujenga maabara then walimu wapewe mishahara yao ili tuweze kuokoa taifa letu
LikeLike
tomeyapokea kwa mikono miwili bali ujumbe ni kwamba”IT IS BETTER TO HAVE HIV/AIDS IN YOUR BLOOD THAN TO HAVE CCM IDEAS IN YOUR BRAIN”THAT IS CHADEMA`S LAW”””””””””””””””
LikeLike
wanaomlazimisha waziri wa elimu kujiuzuru hawatumii busara kwani kujiuzuru kwake hakutafanya waliofeli wafaulu tena suluhu ni kuangalia wapi tumeanguka na kurekebisha kasoro
LikeLike
There must be something in between on the 2012 student’s mass failure our gov. should check it properly why not other years? but the truth will tell by itself
LikeLike
co wote waliofeli hawana akili na jitihada za kusoma napi tucwalaumu waliofeli na walimu wao bali kama kuna tatizo lolote limetokea katika usahishaji tunawaomba mrejee kusahisha tena maana pepa lilikuwa so simple .je serikari mtawapeleka wapi wanafunzi walio feli/?viongozi angalieni hili tukio baya sana
LikeLike
Waziri wa elimu fuatilia shule ya sekondary morogoro Zongomero wanafunzi kila siku ni kulima tu hakuna kuingia darasani unategemea nini kwa wale walio kidato cha pili si kufeli tu jamani walimu wachunguzwe kwa kina.
LikeLike
jamani watanzania wezang 2natakiwa 2boreshe elimu lakn me naona ha2boreshi ila 2nakomoana hususan cc mafukara 2nae tegemea elmu ha2na tegemez
LikeLike
Aa kwakweli mnatuchosha na aya matokeo …………..
2mechoka kukaa nyumbani mtuulumie jamani
LikeLike
jamani mi naona elimu imeshakuwa sio ya watu wote kwani inatolewa kwa matabaka mi naona serekal ingejitahidi kutilia mkazo swala la elimu pia me naona hayo matokeo yamekaa kisiasa kwani haiwezekani robo ya wanafunzi waferi tofauti na miaka mingine hivyo selekali ihakikishe elimu inatolewa kwa wote mfano mimi mock nilipata dvshn one lakin leo matokeo yametoka nimepata dvshn four hii haiwezekani hata kidogo
LikeLike
MAONI YANGU KUHUSU ELIMU TANZANIA; NI KWAMBA
1)ELIMU YA AWALI ITILIWE MKAZO KWA WANANCHI WOTE WA MIJINI NA VIJIJINI, PIA IELEWEKE KUA KILA MTOTO ANA HAKI YA KUPATA ELIMU,
2)PIA SERIKALI IANGALI NA KUWAANDAA WALIMU WENYE TAALUMA YA KUTOSHA NA WENYE SIFA ZA KIUADILIFU NA KIUTUMISHI ILI WANAFUNZI WANAOANDALIWA WANAMUDU MITIHANI YAO.
PIA KUFELI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE WASILAUMIWE WANAFUNZI WALA WALIMU, WANAOFANYA KILA JITIHADA KUELIMISHA WATOTO NA VIJANA WA TAIFA HILI, BALI SERIKALI IANGALIE WAZI SERA ZA ELIMU YETU NA KUPIMA KAMA KWELI INATIMIZWA KAMA SERA ZINAVYOAHIDI.
Kwa maelezo yangu zaidi;0766-496491.
;0689-763324
;0655-496491
Siku njema
LikeLike