TAASISI ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) Kukabidhi Kontena la Vifaa vya Hospitali kama msaada katika Hospitali ya Sumbawanga iliyopo mkoani Rukwa.

 

Katibu Mtendaji wa WAMA, Daud Nasib akizungumza na wanahabari jana katika Ukumbi wa Habari Maelezo, kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uraghibishi WAMA, Philomena Marijani.
TAASISI ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) inatarajia kukabidhi kontena lenye ukubwa wa futi 40 la vifaa mbalimbali vya hospitali ikiwa ni msaada katika Hospitali ya Sumbawanga iliyopo mkoani Rukwa.Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa WAMA, Daud Nasib alisema kontena hilo litakabidhiwa Februani 26, 2013 na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mama Salma Kikwete.

Nasib alisema vifaa hivyo vya hospitalini na vya kisasa vinathamani ya jumla ya sh. milioni 700, vikiwa vimepatikana baada ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika lisilokuwa la Serikali la Project C.U.R.E la nchini Marekani kuchangisha fedha kwa ajili ya ukusanyaji na usafirishaji wa vifaa anuai vya hospitali za Tanzania.

Akifafanua zaidi alisema vifaa vitakavyo kabidhiwa kwa awamu ya kwanza Hospitali ya Sumbawanga ni pamoja na seti nzima ya Mashine ya X-Ray, Mtambo na Kitanda maalumu cha ICU, Mitungi ya gesi ya Oxygen kwa ajili ya huduma ya dharura kwa wagonjwa hasa umeme unapokatika.

Aidha alisema vifaa vingine ni pamoja na mitambo na vifaa anuai kwa ajili ya huduma ya tiba ya kinywa na meno, vifaa vya upasuaji mdogo na mkubwa, Ultra Sound Mashine, Oxygen Concentrators, taa na meza maalumu za upasuaji, mashine ya usingizi na vifaa vingine anuai.Alisema vifaa hivyo ambavyo vimechangishwa katika Jimbo la Arizona nchini Marekani vitaendelea kuwasilishwa kwa awamu katika hospitali kadhaa ambazo zimeteuliwa na WAMA kwa kushirikiana na Project C.U.R.E.

Hospitali zingine ambazo zitanufaika na mpango huo wa vifaa vya hospitalini kwa awamu tofauti ni pamoja na Hospitali za Lugula-Mtwara, Kitete-Tabora, Simiyu-Mkoa mpya wa Simiyu na Hospitali ya Tumbi-Pwani.

Hata hivyo Februari 6, 2013 Mama Salma Kikwete alikabidhi pia kontena kama hilo likiwa na vifaa vya hospitalini kwa Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi.

“Moja ya malengo ya taasisi ya WAMA ni kusaidia kuboresha utoaji na matumizi ya huduma bora ya afya kwa wanawake na watoto na jamii kwa ujumla kupitia uraghibishi na kutoa msaada wa vifaa vya hospitali kwenye hospitali zenye mahitaji makubwa,” alisema Katibu Mtendaji wa WAMA.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s