Lady jaydee: Clouds fm ni wanafiki,wanataka wahongwe ili wapige nyimbo za wasanii Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J”


 

 
 
Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

“Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira”

Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!”

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena “Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng’oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive”.

“Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me”


Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J”
Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa

Advertisements

China’s Xi heads to Congo on final leg of Africa tour


 
China’s new President Xi Jinping was headed Friday to the Congolese capital Brazzaville, the final leg of a three-nation Africa tour that has underscored Beijing’s growing presence in the resource-rich continent.
 
China's president Xi Jinping
China’s president Xi Jinping
 
Deals worth several billion dollars are due to be signed during Xi’s two-day visit to Congo, an impoverished country of four million with significant oil resources.
 
One will finance the building of more than 500 kilometres (300 miles) of highway between Brazzaville and the economic capital on the Atlantic Coast, Pointe-Noire.
 
Xi’s African tour, part of his first presidential trip that began in Russia, has also taken him to Tanzania and South Africa.
 
China’s business boom and its rise to become the world’s second-largest economy has seen financial and trade ties rocket in recent years as it sources many of its raw materials from Africa.
 
But ahead of Xi’s visit to Congo, many expressed doubt that he will bring job opportunities with him, since when Chinese companies set up shop in Africa, they often bring their workers with them.
 
“It’s like we don’t have able hands in Congo,” a teacher at a training college told AFP. “If you import labour when there are no able people or specialists, that’s OK. But they even bring their own chauffeurs. There’s no transfer of abilities.”

Mke wa Rais wa China Mama Liyuan aipongeza taasisi ya WAMA


 

img_6574Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) 

……………………………………………………………………..

Na Anna Nkinda – Maelezo

Mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan amezipongeza kazi  zinazofanywa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kupitia taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ya kuhakikisha kuwa inawainua wanawake kiuchumi na kuwasaidia  watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi kupata  elimu sawa na watoto wengine.

Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Mama Liyuan alipotembelea ofisi ya WAMA kwa ajili ya kuona kazi mbalimbali wanazozifanya  na  kutoa zawadi ya vyerehani 20 kwa ajili ya Umoja wa Vikundi vya WAMA  (UVIMA) na mabegi ya shule 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama.

Mama Liyuan alisema kuwa  kupitia taarifa mbalimbali alizozisoma ameweza kufahamu  kazi na juhudi za Mama Kikwete anazozifanya za kuisaidia jamii na ataangalia jinsi gani anawezea kumuunga mkono kutokana na kazi anazozifanya.

Kwa upande wake Mama Kikwete alimpongeza Mama Liyuan  kwa kuitembelea  Tanzania muda mfupi mara baada ya mume wake  kuwa madarakani  kwani kitendo hicho kinaendeleza  ushirikiano na urafiki uliopo baina ya Tanzania na China ambao upo kwa miaka mingi.

“Ninaomba tuendelee kushirikiana kutatua matatizo yanayowakabili wanawake na watoto wa kike kwani changamoto zao zinafanana Duniani kote na  umuhimu wa kuzifanyia kazi ni uleule”, alisema Mama Kikwete.

Naye Tatu Ngao ambaye ni Mwenyekiti wa UVIMA ambao umepata zawadi za vyerehani 20 vya kudarizi alishukuru kwa vyerehani walivyopewa na kusema kuwa vitawasaidia kuongeza ujuzi, kuinua kipato chao na hivyo kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa ndani ya UVIMA kuna  jumla ya vikundi vya maendeleo 35 ambavyo ni mchangiko wa wanaume na wanawake ila asilimia kubwa ya wanachama wake ni wanawake kutoka kata ya Majohe Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Ngao alisema, “Jambo la muhimu ni  wanawake wajiunge katika vikundi vya maendeleo na wahakikishe kuwa vikundi hivyo vimesajiliwa ili waweze kufikika kirahisi na kujikwamua kiuchumi kwani sisi bila kuwa katika vikundi tusingeweza kupata  misaada mbalimbali tunayopewa”.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Winfrida leonard ambaye ni mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo iko Nyamisati wilayani Rufiji alishukuru kwa zawadi ya mabegi waliyopewa na kusema kuwa yatawasaidia kutunza madaftari kwani wanahitaji kuwa na mabegi.

“Ninaishukuru Taasisi ya WAMA kwa kutusaidia kielimu kwani tunasoma bure  bila ya kuchangia kiasi chochote cha fedha na tunapata mahitaji yote ya muhimu kama chakula, maladhi na mavazi.

 Ninaiomba  Serikali iweze kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ambao wamekosa nafasi ya kusoma kwa kuwakusanya pamoja na kuwapa elimu kama alivyofanya Mama Kikwete kwani watoto ni taifa la kesho”, alisema Leonard.

Mama Peng Liyuan ameambatana na mumewe Rais Xi Jinping nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

SERIKALI YASHAURIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATANZANIA WAISHIO NJE YA TANZANIA KATIKA UWEKEZAJI.


 

images

Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.

…………………………………………………………….

 

 Kamati ya  Bunge  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza  nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.

 Kauli hiyo imetolewa
(leo) na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014

 Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu  zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.

 Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha  wataalamu wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania waishio nje.

 Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya kuwekeza nchini.

 Alisema kuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Atimiza Ahadi, Amkabidhi Usafiri aina ya Bajaji Bwana Bashir Msanda Ambaye ni Mlemavu


 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi msaada wa Usafiri aina ya Bajaji Bwana Bashir Msanda ambaye ni mlemavu wakati wa mwanzo wa ziara yake ya kukagua na kufungua miradi ya maendeleo jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Makabidhiano hayo  ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete kumsaidia mlemavu huyo ,yalifanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU