Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO) Taabani!!

 
YAKUSANYA BILIONI 2.3/- KWA SIKU, YATUMIA BILIONI 5.4/-

Na Josephat Isango

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) limekana kuwepo mgawo wa umeme kwa sasa huku likikiri kuwa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo iko katika dharura na haijarejea katika hali ya kawaida kama inavyotakiwa.
 
Ufafanuzi huu unakuja baada ya gazeti hili kuripoti hali tete ya kifedha inayolikabili shirika hili na hivyo kutishia taifa kuingia gizani wakati wowote.

Hata hivyo TANESCO na serikali kupitia kwa Wizara ya Nishati na Madini wamekuwa kimya kwa muda pasipo kuzungumzia mgawo wa umeme ambao umekuwepo kwa wiki takriban mbili katika maeneo mengi nchini.

Akizungumza jana makao makuu ya shirika hilo Ubungo, jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Felchesmi Mramba, alisema kuwa hakuna mgawo wa umeme kwa sasa na kwamba ikitokea serikali ingetangaza.

Pamoja na kukanusha kuwepo kwa mgawo, Mramba alisema ukweli ni kwamba bado nchi iko katika hali ya dharura na hali ya umeme haijarejea katika hali yake ya kawaida kiasi cha kuondoka katika hali ya dharura.

“Ushahidi wa kwamba bado tuko katika hali ya dharura ni kwamba bado mitambo ya dharura tuliyokodi kupambana na hali ya umeme inaendelea kuhitajika lakini pia mabwawa hayana maji ya kutosha kukidhi mahitaji ya umeme bila kuhitaji mitambo ya matufa,” alisema.

Aliongeza kuwa vilevile miundombinu ya gesi haiwapi gesi ya kutosha kuwasha mitambo yote ya gesi ya megawati 501.

Mramba alibainisha kuwa tangu Julai mwaka 2012 hadi Februari 2013, serikali imetumia jumla ya sh bilioni 231.2 kama ruzuku kwa TANESCO kwa ajili ya kununua mafuta ya mitambo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s