TANESCOtz mmemwachia TANESCO_ awe msemaji wenu Twitter?

 
 
 
 Faida ya kampuni kubwa kutokuwa na kitengo cha kushughulikia masuala ya kampuni kwenye mitandao ya kijamii, ama kuwa na kitengo kilichodorora, matokeo yake ni kama kwa mfano ambapo mtu mmoja ameona ajinyakulie ushujaa koko kwa kutumia jina la kampuni ya Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO na kuunda akaunti kwenye tovuti ya Twitter na kujipachika kazi ya kujibu maswali ya wenye kero na dukuduku zao, vile vile kutoa kauli kana kwamba ni agizo rasmi kutoka TANESCO.

Wapo watu kadhaa, wakiwemo viongozi na watu wanaoheshimika/aminika katika jamii, wameingia mkenge kwa kuamini kuwa wanawasiliana na TANESCOtz bila kujua hii ni akaunti ya TANESCO_ iliyo feki.

Na kwa kuwa Twitter haijaitambulisha TANESCOtz kuwa akaunti rasmi ya kampuni/public figure (verified official account), hilo limekuwa jambo rahisi kuwapoteza watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwasiliana na wahusika.

Akaunti ya TANESCOtz ilianza ku-tweet tarehe 16 Januari 2011 na tweet yake ya mwisho ni Juni 6 ya mwaka uo huo ikiwa na jumla ya tweets 17 tu wakati akaunti ya TANESCO_ imeanza ku-tweet tarehe 28 ya Februari ya mwaka huu hadi tarehe ya pili ya mwezi Machi 2013 ilikuwa tayari na tweets 169.

Bofya screen-shot moja moja zilizopachikwa hapo ujisomee tweets za  TANESCO_

 
Tweets za TANESCO_ hadi sasa TANESCOtz  hawajatamka hadharani kukubali au kukanusha kuhusika na akaunti hiyo. Pengine TANESCO inaamini kuwa wananchi wote wana uwezo wa kutambua kuwa hii siyo akaunti yao. Kutokana na kero za kukatika kwa umeme mara kwa mara na majibu ya TANESCO yasiyoendana na hali halisi majumbani na kazini, wapo watakaoamini TANESCO_ ndiyo akaunti rasmi ya TANESCO na majibu hayo ndiyo majibu yao.

Hivi inafahamika kuwa mtu anaweza kukuburuta mahakamani binafsi au kampuni, kwa kutokukanusha au kukubali maneno yanayotamkwa kwa jina lako?

Naam, wapo watu hupeleka kesi mahakamani kushitaki, si kwa lengo la kupata sifa au fidia, bali kushinikiza na kushurutisha mtu au kampuni kutoa funzo kukubali au kukanusha maneno yanayosemwa juu yake, ili kuweka rekodi sahihi kwa jamii kwa lengo la kuwasaidia wanajamii wasibebe dhana potofu kanakwamba ni kweli na kupoteza kumbukumbu sahihi.

*Imeandikwa na Subi-Wavuti
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s