Kinana safarini kuelekea China.!

 
Na Bashir Nkoromo
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 
Abdulrahman Kinana
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro amesema leo kwamba katika ziara hiyo Kinana atakuwa na msafara wa watu 14, ambao baadhi yao ni Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM, Makatibu wakuu wa Jumuia za Chama na Wenyeviti wa Chama wa mikoa.
 
Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, Dk. Asha-Rose alisema, Kinana na msafara wake wanatarajiwa kufika Guangzhou China keshokutwa, Machi 12, 2012.
 
Alisema, ziara hiyo ambayo ni ya kwanza nje ya nchi kwa Kinana tangu kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba, mwaka jana, imeandaliwa na Chama Cha Kimomunisti cha China kwa lengo la kupata fursa ya viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya vyama na wananchi wa nchi Dk. Asha-Rose alisema baada ya kuwasili Guangzhou, kinana na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao wa Chama Cha Kikomunisti cha China watatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo jiji la Dong-guan, Shenchen, Chengdu, Machi 13-14, 2013, msafara utakwenda jiji la Chengdu, Sichuan, Nanchong na kumalizia ziara hiyo katika jiji la Beijing ambako atawasili Machi 18, 2013.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s